Hivi ni kweli kiwanja kupimwa ramani ya mipango miji ni gharama sana?


Bongo nyoso:

1. Nenda Muhimbili usikie gharama za kitanda, dialysis, MRI, operesheni, mortuary, nk.

2. Nenda TRA usikie gharama za Kodi.

3. Nenda polisi uone gharama za kufanyiwa ukaguzi, uchunguzi, ukamatwaji au kuachiliwa.

4. Wapi kuna la maana?

Ni mwendo wa kula na kuliwa kwa urefu wa kamba.
 
Uko sahihi kudeal na waswahili ni kazi sana.
Hawako ofisini kwa ajili ya kukusikiliza wewe unavyotaka wako pale kwa ajili kukupinga kile unachokitaka ili utumie nguvu za ziada ndio ufanikishe kwa gharama za ziada
 
Makavenga, kuna mdogo wangu mmoja anapenda kuniita hivyo, nikisikia makavenga tu, hata niwe chini ya bahari najua huyu fulani.
 
Sio kauzibe, wanataka wakunyonye kirahisi tu
 
Utapigwq asubuhi ww usipojiangalia
 
kiwanja wakati unanunua ...ulinunulia chini serikali ya mtaa au utaratibu ulikuwaje? hapa ndo kuna chanzo na solution ya tatizo lako
Nilinunua Chini ya serikali ya mtaa
Ila maswala ya kukagua ramani ya mipango miji sikufanya kwa sababu nilikuwa siyajui
 
Na hilo ndio jibu la mwisho.
Hao wengine watampoteza bure.
Hayo yote nimeyaelewa baada ya kufuatilia hati miaka 6.
 
Hakuna ghtrama kubwa bali kuna mizegwe inatengenezwa na hao hao wagfanyakazi wa serikalini ili pesa zikutoke.

Ni wizi na ufisadi mtupu.
 
Nilinunua Chini ya serikali ya mtaa
Ila maswala ya kukagua ramani ya mipango miji sikufanya kwa sababu nilikuwa siyajui
kama ulinunua chini serikali ya mtaa kwa asilimia 75 huwenda hivyo havijapimwa ila vimekatwakatwa na kupangiliwa kwa vizuri pamoja na kuwekwa mipaka( nondo au zege) ila rasmi wizarani hazijatambulika. Hivyo hiyo ndio sababu ya hao watu kutaka kupokea fedha zenu ili waandae mchoro rasmi wa mpango mji kama kulivyokatwa hapo kwenu kisha kuupeleka wizarani kupata approval ndo mengine yaendelee..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…