Hivi ni kweli kuna wanaolipwa na CCM kutokana na kazi ya ku post humu ndani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Ni Mara nyingi nimeskia kuwa zipo ID ambazo zinapewa pesa (7000) Kwa siku malengo ni Kwa ajili ya kuanzisha propaganda jukwaa LA siasa au katika jitihada za uenezi kisiasa . Lakini mimi binafsi nimeshindwa kuamini Kwa kuwa uthibitisho ni mdogo. Napenda niskie kutoka Kwa wanaojua kama hio Habari huwa ni kweli au ni uwongo. Na ni member gani Hao unaweza pia kuwataja ila uwe na ushahidi WA ukweli na sio kufuata mkumbo WA kukurupuka
 
cc Lizabon, Rutashobolwa, Pasco Mayalla
 
Nimefikiria nimeona kuwa wengi humu ndani wameshindwa kuwa wavumilivu kwenye hoja za wengine. Mfano mtu anaweza kutoa hoja Kwa kuwa ye kiitikadi ameonyesha kuwa CCM basi hata kama hoja yake ni nzuri watu wataanza kumchambua mtu na sio hoja Kwa kudai kuwa anapokea posho kutoka lumumba.. Nimepata mashaka juu ya hili. Forum hii watu tunafuata tusiyo na uhakika nayo
 
Cc: lizaboni alishalitolea ufafanuzi ole sendeka kwamba wana vijana wapo kwenye mitandao
 
Wamekutuma au?!
 
Wapo mkuu, japo sio wote, kuna ambao wanapost kwa kusukumwa na imani yao kwa chama ila kuna wengine wanalipwa, hiyo buku saba nadhani wanasema tu ila kulipwa kupo
Na sio Jamiiforums tu, hata mitandao mingine ya kijamii kama Facebook, Twitter, YouTube n.k na hata magazeti pia wapo waabdishi wanaolipwa kumuandika mtu flani

ndio game la siasa lilivyo sio Tanzania pekee bali dunia nzima
 
Yes ni kweli, post ya kuwatukana UKAWA ni buku saba, post ya kumkashifu Lowasa ni buku saba na mia tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…