Hivi ni kweli kuna watu wamewahi kupona kabisa H.I.V?

Hivi ni kweli kuna watu wamewahi kupona kabisa H.I.V?

Atalanta

Member
Joined
May 25, 2022
Posts
72
Reaction score
251
Thread hii haipo kwaajili ya kupotosha au kuhamasisha imanipotofu dhidi ya H.I.V. UKIMWI upo na unaua!

Wapo baadhi ya watu ambao walishawahi kupata H.I.V Lakini Baadae wakaja kupona. Wengine huweka wazi Lakini wengine hawaweki wazi. Wengi wao hupona kwa Kutumia dawa za asili na wengine kwa njia wanazozijua wao. Kwakua Mpaka Sasa hakuna dawa ilyopitishwa inayoweza kutibu ugonjwa huu.

Mfano wakati nipo Mdogo nilishawahi kusikia kua kulikua na Bibi mmoja ambae yeye alikua akitibu H.I.V kwa Kutumia majani ambayo alikua akiyakausha kivulini "Mahali popote ambapo hapana Jua" baadae na kuchanganya na madawa mengine Kisha kupata dawa ambayo mgonjwa atakua anakunywa.

Majani yake siyakumbuki jina kwa saizi ila nahisi ni Mlonge Lakini sinahakika Kama ni yenyewe. Nasikia alishawahi kuwatibu baadhi ya watu. "Kama wapo humu wanaweza wakasema itakua vizuri"

Pia humu JF kulishawahi kuwa na thread zinazohusu watu kupona HIV Lakini nyingi Mods waliziondoa. Kwa manufaa ya wengine Naomba Kama Kuna ukweli kuhusu hizi story za watu kupona H.I.V Basi ziwekwe wazi hapa. Najua wapo wengi wenye uhitaji Naamini kabisa hata Serikali inaweza toa mchango wake ili kusaidia Janga hili. Karibuni ...
 
Vipi umeupata au? Anyway wacha tusubiri waje, ila we endelea tu kufuata maelekezo ya daktari hizi porojo zingine usizingatie saaaaana.

Coz mimi binafsi sijawahi kuskia mtu amepona ukimwi ila nimewahi kuskia mtu ameishi miaka 20 tangu agundue ako na maambukizi.
 
Hapana me nipo salama Mkuu Ila Kuna nyuzi nyingi zilikuwepo humu JF watu wakisema kua wamepona ugonjwa huo.
 
Hapana me nipo salama Mkuu Ila Kuna nyuzi nyingi zilikuwepo humu JF watu wakisema kua wamepona ugonjwa huo.
Labda kwa maombi, coz makanisani humo huwa tunaskia skia watu wanatoa ushuhuda ambao ni ngumu kuuamini kwa watu kama sisi tulio na imani haba.
 
Hakuna aliyewahi kupona kama umeyakanyaga we endelea tu kutumia dawa kwa usahihi
 
Hili gonjwa baya sana limekula sana Familia zetu.

Hakuna nyumba Imepona HIV.
HIV&AIDS PANDEMIC DISEASE.
 
Back
Top Bottom