bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Zimepatikana habri za kutatanisha kuwa ndoa ya UKAWA imevunjika rasmi jana baada ya kuwa na utata na msuguano mkali kuhusu mgawanyo wa majimbo, ruzuku, kuteua mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, kumpokea kigogo toka mojawapo ya vyama vikubwa nchini na kutokuaminiana kati ya viongozi waandamizi wa UKAWA. Kuna habari zilizogaa sana kwenye mitandao ya kijamii juu ya kumpokea kigogo fulani ambao wengi mnamfahamu. Habari hizo zimekanushwa vikali na msemaji wa CDM kuwa ni uzushi mtupu hakuna kitu cha namna hiyo. Leo hii asubuhi kwenye FB imeandikwa kuwa UKAWA imesambaratika rasmi na aliyeisambaratisha ni Mkuu sana Mwenye Heri Slaa. Sasa ninyi mkisambaratika sisi tuliowaamini na kuwategemea kuwa mtaleta mapinduzi tufanyeje turudi tulikotoka ambako wanalumbana lakini wanafikia mwafaka na kuchangamkiana na kuwa kitu kimoja. Yetu macho ninyi mkisusa wengine wala!
Hebu mwenye uhakika na kusambaratika au kutokusambaratika kwa UKAWA atwambie nasi tutakuwa tayari kukanusha taarifa hizi ndani ya JF na FB na kwenye mitandao mingine ya kijamii. Tanzania kwanza, vyama baadae. Nakupenda Mama Tanzania.