Hivi ni kweli mwanamke mwenye ujauzito akila asali mimba inatoka?

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Wakuu poleni,

Hivi katika sayansi ni kweli mwanamke mwenye mimba haruhusiwi kula asali nakumbuka kipindi niko mdogo kuna mama jirani yetu alikuwa ana mimba kuna siku walienda kurina asali shambani kwake na yeye akala.

Sasa ilifika usiku ikawa ameumwa sana, wakamkimbiza hospital na kwa bahati mbaya ilibidi ajifungue kichanga tena kikiwa hakina uhai, sasa kwa maelezo walidai ni ile asali ndo sababu, sasa wakuu naomba kujua hivi hapo kuna sayansi yoyote inayohusiana na asali na mimba.
 
mie nililamba asali sana wala sijapatwa na jambo lolote.
nadhani ni kama zile hadithi za mayai na maini.
 
mie bingwa wa asli na karanga sijui labda mila na mila.mim haipiti siku mbili sijala asali na karanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…