Hivi ni kweli nampenda au nataka kulipa kisasi?

pomo

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
267
Reaction score
33
niaje wana jf, mimi ni kijana wa miaka 28, mnamo mwaka 2002 nilikuwa na mpenzi wangu wa kike alikuwa kamaliza A level na mimi nilikuwa nimemaliza o level na nilikuwa nafanya kazi za vibarua(kazi zisizo na ujuzi).wakati anamaliza shule nilimuahidi nita mnunulia zawadi za sherehe. kwa bahati mbaya sikupata fedha na mawasiliano yalikuwa ni barua kwa wakati huo na sikuweza kumjulisha. matokeo yake ya A level yalipotoka alikuwa amefaulu kwa kupata division 1, baada ya hapo alianza visa na kusema mimi ni bahili na siwezi kupata mwanamke kama nikiendelea hivi. chakushangaza ni kuwa nilikuwa namsaidia hapo mwanzo na bado ninampenda hadi hii leo. kuna siku nilikutana nae(2008) akiwa kamaliza chuo, nilijaribu kumwambia bado nampenda lakini yeye akasema eti wakati ule alikuwa bado mdogo na hakuwa na maamuzi na mimi nataka kumlipizia kisasi, anasema nimpe muda wa kujifikiria. mimi najiuliza ni kweli alikuwa hana maamuzi wakati huo? je amekuwa na jeuri hiyo baada ya yeye kufaulu A level nakuwa na uhakika wa kwenda chuo? na mimi ni kibarua sina muelekeo? mimi sikuwa na nia ya kulipa kisasi
 
Mpende akupendae_asiyekupenda achana nae,....thats how we do
 
Fuata moyo wako..ukweli unaujua ww kama unampenda kweli
 
Pole sana,dunia ndivyo ilivyo tafuta mtu mwingine anaekupenda huyo atakupotezea muda tu
 
Hapo nadhani ali-translate lugha uliyoingilia nayo...jaribu kutafakari tena jinsi mazungumzo yenu yalivyokwenda!!!
 
Hapo nadhani ali-translate lugha uliyoingilia nayo...jaribu kutafakari tena jinsi mazungumzo yenu yalivyokwenda!!!
sio lugha mwana jf, mambo yalikwenda vizuri mwanzo badae akageuka hata nafasi ya kuongea nae hakutaka kunipa
 
Pole sana, Lakini nadhani kulipiza kisasi sio sawa kama yeye alifanya kosa haimanishi na wewe ufanye kosa,wewe kua muungwana na songa mbele na maisha nna hakika Mapenzi sio kwanza wala si mageni kwako,unajua kupenda na kupendwa sasa asikupoteze time.
 

dahhh, unasikitisha sana kaka, basi usilalame sana unamkufuru mungu, ushamshtakia inatosha ...mungu atakulipia kaka.
Pole.
 
mkuu hapo hauna chako...kama vipi kubali matokeo na usiandike barua ya kukata rufaa.
 
Fanya unachoona kinafaa kama ilipangwa awe wako atakutafuta tuu hata kama wewe huna kazi ila kama sio hivyo we endelea na maisha pambana uwe na maisha yako
 
hiyo ishakuwa oversize kwako tafuta size yako vinginevyo utauumiza bureeee moyo wako.
 
Jaribu kumwelewa ni kweli alikuwa mdogo kipindi hicho.Usilipize kisasi kwani maandiko yanatukataza .twaambiwa Kisasi ni cha Bwana.
 
umeambiwa atakupa jibu,unaonaje ukasubiri kwanza?haiwezekani ukutane nae tu,umuambie i lavu yuuuu, nae akuambie i lavu yuuu three? huo ungekuwa uongo.mpe nafasi,muoneshe kama bado ungependa muwe marafiki na usome alama za nyakati utajua cha kufanya.kama mungu kakupangia huyo,muache aseme nae basi.kuwa na subra kaka,mtoto wa kike shurti ajifikirie kidogo asije akageuka daladala!
 
Tafuta kibarua mwenzako mwaego, maana huyu keshaonesha hana haja na wewe, usije endelea nae ukaja juta badae, na ukaishi kama mtumwa wa mapenzi, muda wote huo ulikuwa bado kibarua hukuendelea na shule?
 
Tafuta mke wa kuoa alielingana na level yako ya elimu. Huyo kashamaliza mpaka chuo, wewe fom4. Atakutesa.
 


mkuu hapo kwenye red unamaana mpaka leo ni 2008 au ulimaanisha nini? Siajelewa chochote mzee...halafu 2008 mpaka leo hii 2011 bado ana uhakika wa kwenda chuo au unamaanisha nini mzee? by the way pole mzee...Huyo atakuwa anauhakika wa kuwa mjini ndugu.....kuna wanachuo wenzake na mapapaaa MSOFE....
 

pole sana man .. single ladies they are every where ... just keep your eyes open
 
mwaka huu ni 2011 mwana....alinipa kibuti 2002.....nikakutananae tena 2008 akiwa kamaliza chuo, vp cjaeleweka wapi tena mwana jf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…