Katika rasimu iliyozinduliwa Juni 03,2013 ili wananchi tuijadili na kutoa maoni kwa njia ya Mabaraza ya Katiba; kuna suala la Muundo wa serikali tatu. Mosi; nimejuiliza kwa nini Tume ilipendekeza iwe ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Tanzania? Pili:kwa nini Tume imeona serikali ya Mapinduzi ya Zanziba na Serikali ya Tanzania Bara (ya Tanganyika kimantiki) lazima ziwe na Rais? Tatu;Kwa nini suala la rasilimali halikuweka kinagaubaga?