Ng'wanangwa siku zinakuja hapa si uchonganishi ni ukweli kwanza CCM walikuja na hila zao kuwa CHADEMA ni chama cha kikabila lakini kimewaprove wrong kwa kutwaa ubunge kila kona ya nchi isingekuwa uchakachuaji kingepata majimbo si chini ya 80 yakiwamo majimbo ya Kigoma mjini, Sumbawanga, Shinyanga mjini, Kishapu, Buchosa, Karagwe, Ulanga Magharibi, Segerea, Kigamboni, Mbeya vijijini, Mpanda, Tarime, Geita, Busanda, njombe, chunya na kwingineko kwingi
Halafu pia CCM wajiulize kuwa iwapo wasukuma ni kabila kubwa ambao huwa ni wapole na hawana makuu lakini safari hii Sukumaland imekabidhiwa upinzani katika majimbo ya Nyamagana, Ilelema, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Meatu, Bariadi magharibi (UDP) Biharamulo Magharibi na Bukombe ambayo ni ya wasumbwa jamii iliyomegeka toka kwa Wasukuma wao na Wadakama ni kama kusema muingereza (Englishman) na muayalendi (Irishman) na bado CCM wakachakachua majimbo mengine manne ya Sukumaland ambayo yalikuwa yamenyakuliwa na upinzani majimbo haya ni pamoja na Shinyanga Mjini, Geita, Kishapu na Busanda basi wajue sasa nchi imeamka kama kabila lenye idadi nyingi ya watu ambalo halina makuu limeona CCM haifai hakuna atakayesimamisha hili wimbi la mageuzi CCM watake wasitake siku zao zinahesabika
Naomba nieleweke hapa siongelei ukabila ila najadili kwa kina hali halisi ya nchi ya Tanzania