Mengi huwa nasamehe na kusahau kabisa ,mengine huwa nasamehe lakini huwa sisahau lakini hata siku moja huwa simkumbushi aliyenitenda na mara chache sana huwa nasamehe nusu na huwa namuambia/namkumbusha aliyenikosea mpaka wakati utakapofika moyo wangu ukubalishe huo msamaha.
tumetofautiana sana moto kuna watu hawajui kusamehe kabisa hata akikuambia tegemea maumivu.
mimi mpenzi wangu huwa namsamehe na kusahau pale anapokuwa mkweli.....na analijua hilo.....
zaidi ya hapo huwa sinaga msamaha na subiri kupokea kitu inauma......
Nimependa hapo kwa red Chauro. Basi mi sisahaugi kitu kibaya nilichofanyiwa na mtu ye yote, sema tu huwa najitahidi kutomkumbushia
Sasa huoni kama utakuwa unajipa shida tena mie mtu ambaye hayuko kivile akinikosea huwa namdharau hapo hapo na baada ya muda nasahau kabisa
Kusamehe is deliberate and intentional lakini kusahau inategemea na magnitude ya kosa na limekuumiza kwa kiasi gani.the majority huwa tunaweza kusamehe lakini kusahau kwa wengi inakuwa ni pretence!
Kusamehe yawezekana mziki unakuja kwenye kusahau na ili pezi liwe na afya ukishasamehe si vizuri kukumbusha jambo ambalo limeshapita ukiwa na tabia ya kukumbusha utaonekana unagumu si kwa mwanamke/mwanaume.
Mkuu kapistrano nimependa ulivyoweka hiyo hapo kwa red, kifupi wewe uko kama mimi ktk hili. Ila naomba nikuulize swali kidogo, je unaamini yupo ambaye anaweza kusahau kabisa?
me huwa nasamehe bt % kubwa huwa sisahau bali naignore tu. mf. miaka ileee ya kipindi kileee nliwahi kumfumania bf wangu live bt baada ya km wiki 2 kupita nkasahau sahau tukarudiana na mapenz yakanoga kuliko mwanzo simply b-cos alikubali kosa na kuomba msamaha. kiukweli me mtu akikubali kosa na ku-apologise huwa namsamehe na kuyaacha tu kwa kweli huwa hayasahauliki
Jamani kila mara tunashauriwa kusamehe pale tunapokosewa na wenzi wetu. Tena tunaambiwa usamehe halafu usahau kabisa, then mnafungua ukurasa mpya na maisha yanaendelea!
Swali langu ni hivi, hiki tunachoshauriwa au kuaminishwa (kusamehe na kusahau) kinatekelezeka? I mean, is it realistic or we just pretend?
Binafsi nafikiri kuna makosa ambayo ukitendewa unaweza kusamehe na kusahau na kuna mengine unaweza kusamehe ila hautaweza kusahau (Kama mwanamke kubakwa) na mengine makubwa zaidi unaweza usisamehe wala kusahau (Kama ndugu yako kuuwawa kwa kuonewa au kusingiziwa).
Kiimani unashauiwa hivyo, kusamehe na kusahau na imani hiyo ndiyo inayotulazimisha kupretend kuwa tumesamehe na kusahau ila inapotokea kama mtu amekukosea na ukamsamehe, akirudia tena ni rahisi kukumbuka uliyokutenda mwanzo na kujikuta dhana nzima ya kusahau isiwepo tena.
Kwa kifupi naweza kusema huwa tunajitahidi kusamehe lakini zoezi la kusahau ni kama tuna-pretend tu!