Kuna vitu viwili hapa ambavyo watu wana vichanganya, Kuna Mchumi (Economiser) na Mbahili (Miser). Mchumi ni yule mtu ambaye anatumia rasilimali alizonazo kwa uangalifu mkubwa saana ili mwisho wa siku zije zimletee faida. Kwa maana nyingine mchumi ni yule anaye punguza matumizi yake kwa kuacha matumizi yale ambayo sio ya lazima, Kwa mfano haina haja ya mtu kumiliki pea kumi za viatu, badala yake kama mchumi unanua angalau pea tatu ambazo ni imara na utazivaa kwa muda mrefu, ile pesa iliyo baki katika zile pea saba utaielekeza kwenye mambo mengine ya maendeleo, huyo ndio mchumi. Tukija upande wa pili wa Mbahili (Miser) yeye huyu ni mtu ambaye anachukia saana pale linapokuja suala la kutumia pesa, kwa kawaida yeye hupenda saana kuhifadhi pesa (Hoarding) na hupenda kuishi maisha kana kwamba yeye ni masikini saana. Kwa mfano kuna kabila moja hapa Tanzania (Naomba nisilitaje), yeye anaweza akaumwa saana lakini pale linapokuja suala la kwenda kununua dawa ndio utata unaanza, atasema kuwa hana pesa kabisa na wakati huohuo chini ya godoro ameficha pesa tena za kutosha, sasa huyo ndio Mbahili. Ukiwa Mbahili ni vigumu sana hata kufanya uwekezaji kwa maana yeye suala la kutumia pesa ni sumu kubwa.
Tukija kwenye suala zima la utajiri, hapo ni suala zima la mtazamo, na mimi binafsi nadhani ni bora ukawa Mchumi unaweza ukafikia ndoto zako za utajiri lakini sio Mbahili. Ila naendelea kusisitiza kuwa hilo ni suala la mtazamo.