Binafsi nimechukizwa na tabia au mwenendo wa TATAKI na BAKITA kuwaaminisha wazungumzaji wa kiswahili hususani wa Tanzania kwamba kila neno la sayansi na tekinolojia lazima lipate kisawe chake kwa kiswahili. JJambo hili limejionesha sana katika sayansi ya "computer" na "information". Kwa mfano, neno kompyuta limeshazoeleka tena limekwishatoholewa na wazungumzaji wa kiswahili; wao wamekuja na neno "NGIMBUZI"?
Je, kwani ni lazima kila lugha inayozungumzwa tanzania iwe na msamiati wake uliotoholewa katika kiswahili? Tena wakati mwingine, hupenda kutohoa maneno ya kiarabu. Kwani, kama yakiachwa ya lugha za kigeni ambayo yameshazoeleka kuna ubaya gani? Msamiati wa kisayansi kwa kiasi kikubwa hauna asili ya kiingereza. Kama waingereza, wajapan, wachina na wengine hudiriki kuutumia msamiati wa kisayansi jinsi ulivyo ama kwa kuutohoa kwa nini kiswahili kisifanye hivyo?
Teknolojia na sayansi ni taaluma, na siku zote taaluma haina mmiliki.Tusiwahangaishe na kuwasumbua wazungumzaji wa lugha.Sio kila istilahi ama msamiati wa kisayansi na teknolojia upate kisawe chake katika kiswahili.