Hivi ni lini Tanzanian tutapata katiba mpya?

Mwaipungu

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
293
Reaction score
138
Siasa za Tanzania ni siasa za ajabu sana kuliko nchi yoyote ile. Tulianza vizuri na zoezi la katiba hatimaye bila mafanyikio. Tulianza na bwebwe za kukusanya maoni ya watu ili tuandike katiba yetu ya kwanza toka uhuru wa mwaka 1961. Mm kwa mtazamo wangu huwa siamini kama sisi ni watu huru mpaka siku ambayo mawazo ya watanzania yatapewa kipaumbele na kujumuishwa ktk katiba; watanzania tutaheshimiwa na serekali na kuthaminiwa mana kwa kweli hivyo sijaona kama serekali inaogopa watu bali watu wanaogopa serekali na hii si sawa.

Nanuku kutoka kwa Thomas Jefferson ktk khotuba yake maarufu: "When the government fears the people, there is liberty. When people fear the government, there is tyranny. The strongest reason for the people to retain the right to keep and bear arms is, as a last resort, to protect themselves against tyranny in government".

Sasa basi mm sioni sababu zozote sisi na serekali yetu kushimdwa kuandika katiba ya kwanza toka uhuru wa 1961. Tumekua watu wenye kushindwa kumaliza mambo kwa wakati kwa mfano kabla hata jambo halijakamilika tunahamia kwenye mambo mengine; mm najua ni mbinu za kiasiasa ila sioni sababu ya sisi kushindwa kufanya jambo ambalo litaisaidia nchi yetu kufikia lengo kuu.

Nadhani tunahitaji kujirekebisha na kufanya mambo makubwa. Wazo la katiba kwa EAC lilikuwa letu lkn kenya ilifanya kweli kuleta mabadiliko kwenye siasa yake mana kenya si ya mtu mmoja na hata Tanzanian si ya kundi fulani ni wetu sote watanzania na kwa hilo tunahitaji kuheshimiana.
 
Iliyopo inatosha. Katiba mpya siyo kipaumbele. Viwanda ,kupanua barabara ,elimu bureee, afya nk ndivyo vipaumbele kwa sasa. Ukihoji sana katiba mpya huo utakuwa ni uchochezi.
 
Kweli lkn katiba ni bora kwa sasa tunahitaji tujue haki za watanzania na si ghorofa, viwanda, elimu na afya mana vyote hivyo zimefeli mana katiba ndio muongozo bora kwa serekali. Lkn pia inapunguza mtu mmoja kuwa na nguvu kubwa sana ambayo anaitumia vibaya. Kuna kila sababu kwa Tanzania kupata katiba mpya. Mfano mwanadamu akishimdwa ktk mambo yake hapa duniani huwa anakimbiliza kuomba mungu amfanye wepesi ktk maisha yake sasa sisi tunakimbilia katiba ili itufafanulie nguvu ya mtu inaanza wapi na kuishia wapi.
 
Siasa za Tanzania ni siasa za ajabu sana kuliko nchi yoyote ile. Tulianza vizuri na zoezi la katiba hatimaye bila mafanyikio. Tulianza na bwebwe za kukusanya maoni ya watu ili tuandike katiba yetu ya kwanza toka uhuru wa mwaka 1961. Mm kwa mtazamo wangu huwa siamini kama sisi ni watu huru mpaka siku ambayo mawazo ya watanzania yatapewa kipaumbele na kujumuishwa ktk katiba; watanzania tutaheshimiwa na serekali na kuthaminiwa mana kwa kweli hivyo sijaona kama serekali inaogopa watu bali watu wanaogopa serekali na hii si sawa.

Nanuku kutoka kwa Thomas Jefferson ktk khotuba yake maarufu: "When the government fears the people, there is liberty. When people fear the government, there is tyranny. The strongest reason for the people to retain the right to keep and bear arms is, as a last resort, to protect themselves against tyranny in government".

Sasa basi mm sioni sababu zozote sisi na serekali yetu kushimdwa kuandika katiba ya kwanza toka uhuru wa 1961. Tumekua watu wenye kushindwa kumaliza mambo kwa wakati kwa mfano kabla hata jambo halijakamilika tunahamia kwenye mambo mengine; mm najua ni mbinu za kiasiasa ila sioni sababu ya sisi kushindwa kufanya jambo ambalo litaisaidia nchi yetu kufikia lengo kuu.

Nadhani tunahitaji kujirekebisha na kufanya mambo makubwa. Wazo la katiba kwa EAC lilikuwa letu lkn kenya ilifanya kweli kuleta mabadiliko kwenye siasa yake mana kenya si ya mtu mmoja na hata Tanzanian si ya kundi fulani ni wetu sote watanzania na kwa hilo tunahitaji kuheshimiana.

Mkuu serikali zetu huku makwetu kwa silka hupenda kuogopewa. Sasa serikali iogope watu wake? Thubutu. Kama hilo litapatikana kwa katiba mpya basi tambua kuwa katiba hiyo haitaridhiwa kirahisi na serikali. Hiyo ni lazima ipiganiwe cha kusikitisha labda baadhi ya wapiganaji itabidi walazwe Nairobi kama si kuwa mbuzi wa kafara kabisa.

Katiba mpya haitaletwa na serikali bali inaweza kupiganiwa na wananchi na ikapatikana.
 
Back
Top Bottom