Hivi ni mimi tu sipendi kutumia Ofisi za Serikali?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Binafsi sipendi kabisa kwenda hospital za serikali ukifika watumishi wana jifanya wapo bise kuliko kawaida una jielezea shida yako DR wakiume ana kuangalia kwa jicho
La dharau sana

Ukija TRA hapa sito enda tena namtuma mtu afwatilie nipigiwe simu tu uki ingia ofisi zao wana jifanya kama hawa kuoni kabisa wana kuuliza maswali ukiwajibu wana kukatisha katisha sipend niwe naongea mtu ana nikatisha

Halmashauri uku ndio usiseme kabisa una kaa kwenye bench mpaka una omba poo mtu ana kusahau kabisa wana piga umbea tu

Ni mimi tu au
 
Never say never… siingiagi hosp za serikali,, ni mm na private tena hivi vi polyclinic,, ila Siku ya siku nikapewa refferal to Mt. Meru… kudadeki , nilipata experience mbaya siji kusahau. Niliichukia hadi hosp yenyewe 😀 Nikipita hata round abt ya tembo tu pale nafeel maumivu ya ile siku.
 
Mimi nikiwaga na pesa huwa sitaki kabisa kusikia wala kuyasogelea hayo majengo huwa napenda mambo yangu niyamalizie kwenye maofisi private kwa sababu sipendi kupoteza muda mwingi kubembeleza.
Napenda huduma ziende systematic sio nimepoteza masaa 2 baadae nakuuliza umeishia wapi unaanza kuniletea porojo huwa napandwa na hasira sana,na siwezi kujizuia nikishakasirika neno lolote litakalokuja nalitoa sitojali wewe ni nani
 
Utakuwa tajiri wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…