Hivi ni mimi tu sipendi kutumia Ofisi za Serikali?

Tumia hawa wanasheria wamejaa kibao hawana kazi ndio tunaowatuma tuma kufuatilia documents
 
Ofisi zote za serikali ni za umma,sio za biashara,unakwenda ukiwa huna namna,ndio maana hawajawahi kuwa wakarimu.
Ukikutana na afisa(mtumishi) ktk ofisi ya umma ni mkarimu,fanya uwe unamuombea kila wakati ktk sala zako,na ikiwezekana fanya ajue kwamba umefurahishwa na huduma yake asife moyo.

Sekta tulizoamini zamani kwamba ni za wito mambo sio hivyo tena,ukienda hospitali umedhulika na wabaya au ajali hujitambui,kama hamna wa kukudhamini ktk maelezo unawezakufa wanakuangalia tu.

Mungu atuepushe sana na mabalaa.
 
Wanajifanyaga wapo bise sana na wanajua kulipua mambo
 
Usiombe unatakiwa kuonana na mkurugenzi, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya au tu hata mkuu wa Idara fulani. Hata uwe na appointment hamna rangi utaacha kuona kwa huo mlolongo.

Ila mahali pengine wako vizuri sana accessibility ni kubwa, Mtumishi wa watu unanyimaje watu access.
 
Ndio tabia zao una muuliza umefikia wapi jibu short tu tulia hapo sijui yule hayupo mara huyu amekosea
 
nenda ofc za NIDA ukakutane na majibu.
 
Kipindi cha Magufuli usingeona huu ujinga
 
Una tukanwa vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…