Grand Master Dulla
JF-Expert Member
- Jul 20, 2012
- 411
- 148
Kusema kweli watu wengi wanaweza wasimjue lakini huyu mtu alikuwepo na bado yupo na ataendelea kuwepo. Si mwingine ninayemzungumzia hapo zaidi ya Abdulrahman Babu, kipenzi cha watu mwanamapinduzi wa kweli, shujaa na mtu mwenye akili nyingi sana na maono ambaye sijawahi kupata kuona mfano wake na mbadala wake.
Babu ni msomi aliyebobea na mwanauchumi mzalendo kwa bara lake. Sitaki kuongea mengi ila kila nikikaa nikifikiri bado nadhani nchii hii inahitaji kumfanyia kitu huyu msomi. Kumbuka reli ya TAZARA, kumbuka urafiki wetu na China na mengineyo mengi aliyoyaanzisha.
Kwa kifupi ni kwamba ili sisi tuweze kuendelea na kubarikiwa ni lazima tuonyeshe shukrani kwa watu kama hawa na wengine la sivyo mafanikio tutayasikia kwenye redio tu.
Nawasilisha...