Hivi ni sahihi kuipiga makofi msibani?

mipango99

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2022
Posts
623
Reaction score
903
Leo nilikuwa kawe kwenye msiba wa Askofu Jonathan kwanza nilikuwa nahuzuni kweli moyoni.

Mpaka pale alipo panda Askofu mkuu wa makanisa ya Calvary akatoa maneno ya kuchangamsha kusahaulisha msiba kidogo moyo ukalainika huzuni ikapungua

Katika kuendelea endelea pale akatoa maneno mazuri mazuri watu wakajisahau wakaanza kumtunza na hela sio mbaya

My point nipale mkuu wa mkoa alivyo panda watu wakaanza kuipiga makofi. Je, ni sahihi kwenye msiba kupiga piga makofi sio kero kwa wafiwa kweli nimeshangaa
 
Msibani huwa hatuahangaik na aliye kufa bali huwa tunahangaika na waliobaki

Kwahiyo waliobaki siku zote huhitaji faraja na kanisa kazi yake ni kutoa faraja

Msibani siyo sehemu ya kuongeza majonzi kwa wafiwa bali kupunguza majonzi
 
Misiba ya siku hizi watu wanapiga pombe kama harusini, sasa ikitokea pombe zimekwisha halafu muombolezaji mmoja akasimama nakusema anaongeza kreti 20 za bia kwanini asipigiwe makofi
 
Kupunguza kivip..kutoa maneno ya kiucheshi watu wakicheka ndo wakupigie makofi..
 
Misiba ya siku hizi watu wanapiga pombe kama harusini, sasa ikitokea pombe zimekwisha halafu muombolezaji mmoja akasimama nakusema anaongeza kreti 20 za bia kwanini asipigiwe makofi
Hii imeenda..
 
Mzee inaonekana ukiwekewa 1+1 = ?, Alama zikawa 100 utafeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…