rbsharia; Kwa kawaida hapa nchini kwetu tumezoea kusema mimi nafanya kazi huku napiga shule. Na hapo hapo tunaambiwa kuwa mshika mawili moja humponyoka.Kwa upande wangu mimi naona sio sahihi sababu ili jambo lifanyike kwa ufanisi linahitaji muda mwingi zaidi. Je, mambo mawili kwa wakati mmoja mtu utaweza kujigawa 50% kwa 50% ?
Mkuu, Inawezekana kabisa, mara nyingi kwa graduate level nimeona wengi wanafanya hivyo.Kufanya vizuri kwenye masomo haijalishi kuwa upo full time, unaweza kufanya kazi na bado ukafanya vizuri kwenye shule yako pia. Ni kupangilia mda na kujima usingizi kidogo mambo yanaenda.