Hivi ni sahihi Mwanaume kumsaidia Mkewe kazi za ndani?

Hivi ni sahihi Mwanaume kumsaidia Mkewe kazi za ndani?

Sharobaro la jf

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
237
Reaction score
325
Hivi ni sahihi mwanaume kumsaidia kazi za ndani mkewe kama kuosha vyombo, kupika na kuogesha watoto?
 
Maisha Ni kusaidizani mzee fanya lakini kwa furaha yako mwenyewe sio kuendeshwa huo utakuwa zuzu
 
Upendo wa kweli unaweza kutenda zaidi ya hayo...
 
Ndio. Ni sahihi. Nyumba Ni yenu, watoto Ni wenu, shida Iko wapi? Na Kazi anafanya nje mshahara analeta anakusaidia pia na uanamke haupungui.
 
Yap ni muhimu sana kwani ukipika au ukamuogesha mwanao kuna shida gani mimi vyombo tu ndo siwezi osha ila kupika na kuogesha watoto nafanya
 
Hivi ni sahihi mwanaume kumsaidia kazi za ndani mkewe kama kuosha vyombo, kupika na kuogesha watoto?
Sahihi kbs,hasa mkiwa hamna dada. Me huwa nawaosha makidi wangu wanne,moja akimaliza anenda rum kwao mke anawavalisha,naosha vyombo,kupika sana sana kukaanga mayai 🤣..nafua of koz na mashine..nazingine zingine,ila kupiga deki kwa kweli nimeshindwa.. 😀Mke ni mtu wa kumsaidia sana kila uwezavyo
 
Hasa mkiwa hamna msaidizi, akiwepo msaidizi unafanya for leisure. Lakini kama hamna msaidizi kwa nini msisaidiane kazi za ndani, watoto, nyumba na kila kitu ni vyenu, kwa nini iwe nongwa kusaidiana majukumu ya ndani!
 
Msaidie pale utakapohitaji wewe mwenyewe kufanya hivyo isiwe mazoea kila siku...ukifanya mazoea kila siku utaumbuka siku moja wanawake ni wapuuz baadhi ya muda.
 
Ni vizuri sanaa kushiriki/kusaidiana shughuli za ndani na mwenza wako si tu itawafanya kuwaweka karibu lakini as a man itaonesha jinsi gani unamjali mwenza au familia yenu kwa ujumla (being responsible ).

Unfortunately sio wanawake/wadada wote wenye kuona thamani ya jambo hilo 👆, i met with this girl sio tu alikuwa ana take advantage lakini baadae akaanza kuona kama ule ulikuwa wajibu wangu, like usipomsaidia au kufanya nae baadhi ya kazi basi atakununia na asizungumze kabisa na wewe 😂😂, kibaya zaidi zaidi siku nimekaa na rafiki zake wananihadithia jinsi gani nilivyokuwa mzuri wa kukorofisha jikoni na ninavyowajibika kwa shughuli za nyumbani, means huwa anawahadithia almost vitu vyote ninavyofanya ndani 😤, guess what, kikichofuata baada ya hapo ni spana tu 🔧🛠 tu.

Sipendagi ujinga mimii.
 
Back
Top Bottom