Kwa boxer basi hakikisha unatumia oil aina moja, yaani usiwe unabadilisha badilisha brand ya oil. Pia hakikisha kila unadilishapo oil basi badiki na oil filter, Yote hayo fanya kila baada ya km 1000 ili kukipa chombo uhai mrefu.
Kingine kama pikipiki yako ni kwa commercial use especialy bodaboda basi kumbuka kui grease pikipiki kila baada ya miezi 3 pamoja na kusafisha air cleaner.
ZINGATIA : kwenye uendeshaji usipendelee sana kutumia gia ndogo kwa mwendo mrefu hadi engine inalalamika, hakikisha uki flow gear kwa kuzingatia mlio wa engine na kuweka gia stahiki inayoendana na mwendo.
Ukizingatia hayo chuma itakaa hata miaka 10.
Mie boxee yangu inamiaka 4 sasa, ni ile ya gia 4 lakini ukichukua mo boxer leo pale kariakoo au tvs ukasema tuwekeane ligi basi hutaisogelea wala hutaiona.