Tangu tunakua, tumejikuta Waafrika wengi tuko kwenye tamaduni ya aina hiyo. Nilikuwa nasoma vitabu vingi vya zamani, vilikuwa vikisimulia kuwa ilikuwa inafikia level ya mtoto wa kike anapozaliwa hapo hapo anakuwa "booked" kuja kuolewa na kijana au mzee fulani!
Lakini ki ukweli, huu ni kama utamaduni tu wa zamani ambao kimsingi huufanyi kazi kwa nguvu ile ile kwa vijana wa kizazi cha sasa. Ki ushauri, niungane na huyo mchangiaji hapo juu kuwa suala muhimu ni kupendana kwa dhati. Suala la umri lisiwe kikwazo sana ingawa pia unatakiwa kuwa na mipaka ya huo utofauti wa umri.
Si busara we kijana kuoa/kuolewa na kibabu/kibibi. Kwa mtazamo wangu naona tabia, interest na hulka zinaweza kupishana na hivyo kuleta migogoro isiyo ya lazima.