Sio TCU Ni UDOM wenyewe pamoja na Serikali(nitaandika kile ninachojua), ingawa unasema watu hawajafanikiwa, wapo watakaofanikiwa ila kwa idadi ndogo, labda nikwambie tu hivi UDOM, ilipoanza na intake ya kwanza ilikuwa ya watu wachache sana, pia intake ya pili, intake ya tatu ilitia fora..mtu asikuambie muulize yeyote aliyepata kuwa pale na kuiona intake ya 2009/10.
Hii intake iliwapa shida sana. wakufunzi walikuwa wachaache wanachuo kibao! ikawa sasa hata Thietre watu wanasoma wamekaa mpaka miguuni mwa Lecturer, wakati mwingine hata lecturer alikosa hata pa kusimama, amini usiamini ili mtu awai kipindi cha saa 2 asubuhi kuna wakati iliwalazimu watu kuamka saa kumi na moja na bado muda huo unakuta no chance, unajirudia kulala.
sasa hili tatizo nadhani wakaliona, na ninadhani walilichukua kama changamoto, katika prospectus ya UDOM ya mwaka 2011/12 kwenye utangulizi inasema, wamekubalina na Serikali ku maintain few number of students for couple of years so as to ensure Quality education.
Ile nyomi iliyochukuliwa musimu wa 2009/10 ndiyo sasa inaondoka mwezi huu (wanamaliza mwaka wa tatu) wengi wao, ispokuwa baadhi ya kozi za miaka mi 4 kama sheria(wachache).
Hivyo kwa tafsiri nyepesi ni kuwa lile zoazoa la UDOM tusilitegemee tena kwa hivi karibuni, watakaopata chance ni wachache kwaaajili ya mpango wao huo wakuwa na wanafunzi wachache kama walivyokwisha onesha ili kuhakikisha Elimu Bora.
Labda kwa kuongezea tu ni kuwa hawa wanaoondoka sasa ndo pioneers wa mwisho katika series (wanaitwa magreda) ya kujenga barabara. will be the 3rd output. walioko mwaka wa kwanza na wa pili sasa ni namba ndogo sana na iliyoingia kwa vigezo haswa tofauti na ma pioneers, the incoming ndo nadhani ushaona na vigezo huko. more tight.