Hivi ni ‘tuzo‘ au ‘tunzo‘?

Hivi ni ‘tuzo‘ au ‘tunzo‘?

The Dude

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
1,029
Reaction score
459
Kuna matangazo ya kili music awards..watangazaji wanasema tuzo za kili wakati wengine wanasema tunzo.

Hii imezua mjadala na ubishano usio kifani na wenye mashiko baina ya mimi na wana familia yangu hapa.

Neno sahihi ni ‘tunzo‘ ama ‘tuzo‘..?
Ni hoja nzito,kuna wanaosema neno fasaha ni ‘tuzo‘ halikadhalika kuna wanaosema ni ‘tunzo‘
Je,wadau,mnaonaje? Lipi sahihi?
 
Neno fasaha ni TUZO,unapata tuzo au unatuzwa(award\awarded)
Tunzo unapata kutokana na matunzo(taken care of)
Mfano nani anaweza kunitunzia gari yangu nikiwa safarini
 
Neno fasaha ni TUZO,unapata tuzo au unatuzwa(award\awarded)
Tunzo unapata kutokana na matunzo(taken care of)
Mfano nani anaweza kunitunzia gari yangu nikiwa safarini

.
Naona unataka kumpoteza mwenzako!

Maneno yote ni sahihi!


Kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI


tuzo nm [i-/zi-] prize, reward.

tunzo
nm [li-/ya-] reward, award.

.
 
.
Naona unataka kumpoteza mwenzako!

Maneno yote ni sahihi!


Kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI


tuzo nm [i-/zi-] prize, reward.

tunzo
nm [li-/ya-] reward, award.

.

Hapa nimepata shule ya kiswahili nilikuwa nafikiria kama mchangiaji wa kwanza.
 
Na hata wale wanaofanya maonesho au michezo au kuimba tunapowapa hela si husema tunawatunza au tunawatuza?
 
Back
Top Bottom