Hivi ni ukoo wetu tu tuko hivi au na wengine mna experience upuuzi kama huu?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Miaka kadhaa iliyopita ndugu yetu katika ukoo alipata ajali mbaya ya barabarani na ilihitajika matibabu ya dharura lakini yenye umakini, na kama mnavyojua matibabu ya umakini kwa nchi hii ni yakulipia. Ndugu tulikusanyana ili kila mtu aweze kutoa mchango wake kufanikisha matibabu hayo.

Michango ilikua ya kusuasua sana, na kwakweli kasi ya utolewaji wake ilikua hailingani na mahitaji ya udharura ya mgonjwa, kwani baada ya muda mrefu wa kikao na kuhamasishana bado hela zilizopatikana zilikua kidogo na zisingeweza kufanya mgonjwa apelekwe theater.

Nilipoona mambo yako hivyo na hisia za maumivu anazopata mgonjwa nikaanza kujitolea kutangaza kuchangia kiasi kikubwa, baada ya sekunde chache nikaungwa mkono na ndugu wengine watatu waliochangia kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi pesa ya matibabu ikapatika.

Siku ileile nikapata wito kutoka kwa mama yangu mzazi kua kesho yake niende kwake ananiita, na mimi nikaamua kwenda siku ileile bila kusubiri kesho. Nilipofika alinionya sana kwa kitendo nilichofanya cha 'kutangaza' kutoa pesa vile mbele ya kikao japo kilikua cha wanandugu. Akanambia watu sio wazuri mwanangu japo ni ukoo wenu, na maneno meengi ambayo niliona kama maneno ya kizee tu. Risala ilikua ndefu na yenye kunisisitiza lakini mimi nilimsikiliza Bi mkubwa kama ada tu huku yakiingia sikio moja na kutokea jingine

Wiki moja baadae nilishangaa baada ya kukutana hospitali(mgonjwa alikua kashafanyiwa oparation) na mmoja kati ya wale ndugu waliotoa mchango mkubwa, akaniambia baba yake hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujitolea 'hadharani' kutoa mchango. Akamwambia bora angefanya siri au angelipa moja kwa moja hospitali kimyakimya. Japo sikumwambia kua na mimi nilikabiliwa na hali kama yake lakini wote tukakubaliana kua wazazi wanazeeka na visheria vyao ambavyo havisaidii jamii.

Miezi kama kumi na nane baadae nilipatwa na mshituko. Nilikua naongea na dada yangu binamu ambae alinimwagia maelezo meengi kuhusu tukio lile la kuchanga siku ile. Eti watu hawakulipokea vizuri japo walijifanya wameshangilia tulipokua tumetangaza michango yetu. Dada binamu akaanza kunitajia kwa majina ndugu ambao wanauwezo kuliko hata sisi tuliotoa michango mikubwa lakini kila mmoja alikua anasubiri atoe kiasi kilekile ambacho watu wote watapangiwa kutoa! Akanihadithia na maneno watu waliyokua wanayasema pembeni na baada ya kikao eti tunajifanya tunaazo na mengine mengi ya kebehi na kuvunja moyo sana!

Kipindi kirefu kilikua kimepita toka mchango ule na yale mazungumzo na dada binamu lakini kwakweli niliumia sana kwa maneno yale na nikiri yaliniathiri sana na yalinibadilisha kabisa mtazamo na approach yangu kwenye shughuli za kifamilia. Nilikua nahisi watu hawaoni mahitaji ya watu kwenye ukoo lakini unashangaa huyo unaedhani anauhitaji badala akufuata umpe ramani za michongo ya town yeye anakusema unapofanya kitu positive! Najiuliza hivi ni ukoo wetu tu ndio tuko hivyo au ndugu zangu nanyie mshawahi ku experince kitu kama hicho?
 
Majungu yapo kila ukoo we shiriki sehemu unayopata amani
 
Yawezekana mlitafsiriwa kuwa mmejitanguliza ninyi badala ya wazee wenu. Katika uongozi hasa unapotaka kufanikisha jambo pasipo nitafaruku ya baadae lazima wakati mwingine tutumie falsafa na itifaki mkuu.

Wivu na vijicho vipo kwa tulio wengi. Sifa nazo na umaarufu katika jamii bado vinaleta shida japo hutajwa kwa jina LA heshima.

Yaani hamkuwaheshimu wazee wenu mkajiinua ninyi wadogo.

Wakati mwingine tujitahidini kuwatumia wanaowazidi umri ili hali ya hewa isichafuke, hasa kwenye shughuli zinazofanana na hizo.

Uliza ujiji ama mwanawota ni maeneo yanayofanana na mazingira uliyokutanana nayo mtoà mada. Huko vijana huwa wanajulishwa( na wazazi wao) kabisa kwamba hata likizo wasifike. Sembuse kutoa mchango mkubwa tena kwa dharau mbele yetu sisi wazee? Lazima tu tutakunyesha ama kukushikisha adabu.Teh Teh Teh
 
njoo Tabora uone ndo maana hata maendeleo hakuna ukionekana unaanza kuyamudu maisha utarogwa na mkoa wote wageni ndo wanatoboa huku
 
Na ndio wakwanza kulia kwa uchungu km mgonjwa ameenda mbinguni.
 
Hyo ipo sehemu nyingi sana

Ndugu wakishakua na kipato yan wate wanajitegemea linapokuja swala la kumsaidia fulani lazima washikane uchawi

Sijui kwa nn binadamu tumeumbwa na roho za namna hii!
 
Koo nyingi za kiafrika zina roho za kishetani, jirani au mpita njia hawezi kukuroga lakini damu yako haichelewi kukupa jini.
 
Koo nyingi zipo hivyo.

Ndugu wanapenda kuona huna kitu, na ukipata kitu wanajitahidi kukutafuta lawama ilimradi uonekane wewe hufai.

Enzi unasota hakuna hata mama mdogo wala shangazi aliyekujulia hali wala kukuongezea ada ya shule, Sasa pata kazi uone lawama.

Utasikia yule mtoto ana roho mbaya hapigii mtu simu, wala hatembelei mtu.
Wanasahau wakati unasoma kuanzia Std 1 mpaka huko vyuoni hakuna aliyewahi kuulizia hivi flani yuko wapi au anasomaje na hali ngumu aliyonayo?

Mi ndugu zangu nachagua wa kusaidia, wengine wanafiki sana. Kama ndugu hakua na time namimi wakati nasota basi hata mimi sina time nae wakati ninapopata mkate.

Jino kwa jino tu[emoji34][emoji34]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…