Hivi ni Vitabu Muhimu Ambavyo Unatakiwa kuwa umevisoma hadi sasa
1. The Road Less Traveled cha M. Scott Peck
Kitabu hichi naweza kusema ndio kitabu Babu cha vitabu vingi kuhusu mafanikio ya mtu na kujiongeza. Ni kitabu kitakacho kupa balance na self esteem katika maisha yako.
2. The Things you think you can not Do by Gordon Livingstone, M.D.
Ni kitabu kizuri kinacho kupa nguzo muhimu za kuushinda woga wa kufanya kitu maishani mwako. Mwandishi wake ni Psychiatric doctor ambae kwa muda mwingi alikua akihudumia watu wenye simanzi na woga. Ni kitabu kitakacho kupa nguvu, Ujasiri, na mwamko wa hali ya juu.
3. The Magic of Thinking Big by David Schwartz
Schwartz katika kitabu hiki amewapa wasomaji njia muhimu na hatua za kupitia ili kufanikiwa. Ameongelea jinsi ya kufanikiwa katika kazi zako kwani hahitaji kuwa msomi sana ili kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yako.
4. How to Win Friends and Influence People by Dale Carnegie
Ni kitabu mashuhuri sana na kimesomwa na watu wengi ambapo mwandishi wa kitabu hiki ametumia ujuzi wake wa kuelezea story ambazo zinaonyesha ni jinsi gani unaweza kufanikiwa kupitia mahusiano na kujuana na watu mbalimbali.
5. The Richest Man in Babylon by George S. Clason
Naweza nikasema hiki ni kitabu nguli katika maswala mazima ya kusimamia matumizi na mapato. Kina page 145 tu lakini ni kitabu kizuri na kilicho jawa maarifa ya kutosha katika maswala mazima ya fedha.
6. Quitter by Jon Acuff
Hiki ni kitabu muwafaka kwa wewe unayetaka kufanya mabadiliko ya maisha yako kutoka kwenye kazi za kuajiriwa na kuwa na kazi ambayo umekuwa ukiita kila siku. Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya vitu ambavyo wamekuwa wakivipenda maishani lakini wanajiuliza kama vitawalipa ama la, basi kitabu hichi kitakupa mwongozo na majibu ya maswali yako.
7. The Art of War by Sun Tzu
Hiki ni moja kati ya vitabu vikongwe vya mbinu na mikakati ya kijeshi, Lakini kitabu hichi kimeweza ku unda mikakati ya kibiashara pia.
8. Rich Dad, Poor Dad by Robert Kiyosaki
Kitabu hichi kilichoandikwa na Robert kiyosaki ni moja ya vitabu mashuhuri kitakachokupa maana halisi ya juu ya kuwekeza kipato chako hata kama ni kidogo lakini kwa mafanikio makubwa
9. Economics in One Lesson by Henry Hazlitt
Kitabu hiki kina chapter fupi sana zinazoelezea maana halisi ya uchumi. Mimi nilibahatika kusomea uchumi katika level ya advanced level na hata degree yangu ya kwanza ni ya uchumi. Katika kitabu hiki msomaji utaweza kupata kujua concepts mbalimbali za economics kwa ufasaha zaidi kwani kimelezewa kwa ufupi na kwa mtiririko unaoleweka hata kwa wale ambao hawakusoma economics.
Ukitaka kujua ni namna gani unaweza kuvipata vitabu hivi basi usisite kunijulisha kwa kuniachia comment yako hapo chini au wasiliana nami kupitia
chapisha.com hapo ndio home! :A S wink: