Hivi ni vyakula vinavyofaa kuliwa kila siku ya maisha ya mwanadamu.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
HIVI NI VYAKULA VINAVYOFAA KULIWA KILA SIKU YA MAISHA YA MWANADAMU.

''LET FOOD BE THY MEDICINE AND MEDICINE BE THY FOOD''

 
Ungetuchambulia kimoja kimoja hata kwa majina na umuhimu wake maana wengine picha mpk tuvae miwani halafu tumeisahau nyumbani
Kula kila siku Mboga za Majani,viazi vitamu,Viazi mbatata,ndizi,Matunda ya aina zote kwa ujumla Vyakula vinavyolimwa katika ardhi. Usile Vyakula vya Maviwandani Vyakula vinavyo tengenezwa kwa makopo. Pia usile chizi,mtindi.chips, maziwa na nyama za aina zozote, Pia usile Soda za aina zozote zile Askrim na Juisi za Maboksi usile. Kula samaki fresh wa baharini au kwenye maziwa. Utakuwa na aafya bora. Punguza kula vyakula vyenye madini ya wanga na protini. Kwani sio vizuri kiafya yako.
 
Vinaboa vimejaa mirangi rangi ya sisiem!

Sent using Jamii Forums mobile app
MKUU İingawa Hivyo Vyakula vinakuboa kwa rangi yake ,lakini ndio vyakula vyenye kuleta afya ya mwili wako.Kuliko kula vyakula vingine visivyo leta afya ya mwili wako zaidi ya kukuletea maradhi mwilini. Kma hivi hapa chini vyakula vyenye kuleta maradhi mwilini mwako angalia picha hapo chini.

 
Vipi kuhusu ugali, wali, ngano, mihogo, nk
Matunda ni mazuri lakini hayatoshi kuwa chakula...yaani ni machache, ila ndo vyakula halisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kuhusu ugali, wali, ngano, mihogo, nk
Matunda ni mazuri lakini hayatoshi kuwa chakula...yaani ni machache, ila ndo vyakula halisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kula hakuna shida.

VYAKULA HAVIFAI KULIWA NA WANAUME MARA KWA MARA...

Watalamu mbalimbali wa masula ya afya wameeleza ya kwamba ipo haja kubwa sana kwa wanaume kuacha kula baadhi ya vyakula ili kuweza kuyazuia madhara ambayo nimeyaeleza katika Makala haya, kwani endapo utaendekeza kula vyakula vya aina hii, kuna uwezekano mkubwa afya yako kuwa matatani.

1.Chumvi ya mezani

Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile [aluminium silicatea]huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.

2. Popcorn

Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ˜Diacetyla kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho Perfluorochemicalsâ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD). Hivyo ni vizuri kuacha kula popcorn

3. Mkate mweupe

Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.

Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

4. Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume

Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu wakahimizwa kutumia mafuta ya namna hiyo.

Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume. Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya canola na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.


5. Pombe: Punguza kunywa pombe au acha kabisa kuzuia kuota matiti

Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.

Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.

Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama wanawake.


6. Chips: Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele

Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku. Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.

Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.

Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika moja kwa moja.
 
Hivi tunawezaje kukwepa hivi vitu, zaidi ya kuvipungunguza, sisi wa bara chumvi ya baharini tunaitoa wapi, tutumie mafuta gani nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tunawezaje kukwepa hivi vitu, zaidi ya kuvipungunguza, sisi wa bara chumvi ya baharini tunaitoa wapi, tutumie mafuta gani nk

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia Mafuta ya Zaituni au Mafuta ya Nazi,Mafuta ya parachichi,Mafuta ya zabibu,mafuta ya Ufuta na pia Mafuta ya samaki ndio mafuta hayo yote hayana madhara kwa afya ya binadamu.

Oils
Olive Oil (Do not cook) Mafuta ya Zaituni usiyapike unaweza kunywa
Coconut Oil (Do not cook) Mafuta nazi usiyapike unaweza kunywa
Grape Seed Oil Mafuta ya Zabibu Tumia kuyapikia kwenye chakula.
Sesame Oil Mafuta ya Ufuta Tumia kw akupikia chakula.
Hempseed Oil Mafuta ya mbegu za bangi yanapatikana ulaya au amerika sio afrika.
Avocado Oil Mafuta ya Parachichi.
Dr. Sebi Approved Organic Oils & Butters Combo Package-Brazil-Nut, Sesame, Hemp, Virgin-Olive, Avocado- Brazil-Nut-Butter, Walnut-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…