Hivi nini maana ya Serikali 2 au 3?

jogoolashamba

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
348
Reaction score
71
WaTz janja ya nyani kwelikweli . Utaona watu wazima wa Bara wakilonga eti wana Serikali 2. Lakini ukiangalia kwa undani ni raia wa Zenj ndiyo wanatawaliwa na Serikali 2, yao na ya Muungano. Bara wana Serikali 1 ya Jamhuri ya Muungano. Utata huu wa watu wazima kuendelea kutumia maneno yenye kumaanisha hata jambo lisilokuwepo ndiyo asili yetu, migogoro haishi na kila wataalam wanapojaribu kuchanganua kiini cha mgogoro wanakufa ghafla. Professor Chachage na sasa Sengondo Mvungi.

Wazenj hawana noma kwani kwao wana chao kwanza ambacho hakiingiliwi na Bara. Bara je? Mwinyi alipokuwa Rais wa Tz aliwahi kutangaza wazi kuwa alikuwa amepewa kutawala Bara, Mzenj anatawala Bara. Masikini wote Bara hawakutaka hata kuuliza maana yake, walielewa lakini nani amvishe paka kengele? Mkubwa mmoja mpaka alifunikwa kanga kwenye sherehe ya hadhara, kama ishara ya kuwa mwandani wa wageni waliokuja kutawala nchi.

Hivi wote ni kasoro hatuelewi maana ya SERIKALI 2 TULIZONAZO, au huko juu hawana shida ya kujua maana kwa sababu wao malengo yao yanafanikiwa kimaisha?


Ili Bara wafanane na Zenj basi au sote tuwe na Serikali 1 ya jamhuri, au tatu kama wanavyosema wahenga, ya Bara isiyojuana na WaZenj, ya Zenj isiyojuana na Wabongo (ipo tayri) na ya Muungano ya wote Wabongo na WaZenj. Hivyo ndiyo Zenj watakuwa nazo 2 na Bara nao 2. Ni ujinga kujiita WABONGO huku tunaishi kama majuha ya kusukumwa na kwenda tu. Mimi mpaka natia mashaka Sengondo Mvungi wamemwondoa kwa sababu ya msimamo thabiti wa kutaka Serikali 3. Alikuwa msomi huyu na ushawishi wake ulikuwa maridhawa.

Mchezo wa "Ngamia kuingia ndani ya hema" ndiyo uliowashinda akina Njelu Kasaka na G8, la kushangaza WaZenj ndiyo wakapinga Bara kuwa na Serikali yao karibia wazipige kavu Bungeni.Bara anayekataa Serikali 3 basi anataka serikali 1, akitaka 2 nadhani akapimwe akili kwa "kuingiza ngamia ndani ya hema lake" mchana kweupe, au kalewa huyu hajui analolisema hivyo hafai kutusemea.
 
Ni muhali kujiandikia jibu la hoja yako mwenyewe, lakini najuta hata kuandika ukweli. WaTz wagumu kwelikweli. Ukiwaita janja ya nyani wanakununia, lakini kila kukicha ni yaleyale ya kuzua na baadaye kufunika.

Tufunike hadi lini na kuandika mazuri wakati ni Muungano huo huo ndiyo tunausemea? Kiapo cha Julius kilikuwa: "Nitasema kweli daima, uongo kwangu mwiko". Pamoja na siasa kuwa na urongo kibao, urongo ni kasoro ya kuishia kufunika matatizo lakini yakabaki yanakera watu lakini huku yakizuia ukweli.

Mimi nasema Serikali 2 ni kiinamacho kinachoshangaza hata mataifa ya nje! Mpaka wanasema kuwa Wabongo tunang'ang'ania muungano ili tusiitwe Tanganyika. Wakati sisi tulijitosa wazima ndani ya Muungano na kusahau jina la Tanganyika wazenj bado wana Zenj yao, pamoja na Unguja na Pemba. Kuwaita Tanzania Visiwani na sisi kujiita Tanzania Bara wao wanaona sawa tu lakini kwetu sisi, kwao ni wazenj.

Tusipokubali mabadiliko kwa kusema ukweli wa Julius tutakuja kupata kizazi kisichokuwa na uelewa wa mzengwe gani unaleta uongo fulani halafu wazee wa kuutoa mzengwe husika hadharani hawapo. Kizazi hicho kitakuwa cha wa TZ lakini wenye matatizo yasiyojulikana yametokea wapi.

JK acha hata kwenye MaBlogi watu waandike mabaya na makosa, mema hayakosolewi, ni mabaya na makosa ndiyo hukosolewa ili kuleta mabadiliko kwenda kwenye mema. Kumpa mpitanjia maji ya kunywa haihitaji kuandikwa kwenye Blogi lakini thubutu umnyime, mtajulikana kabila la Wakwere wote mna roho mbaya. Hayo ndiyo maisha na maisha ni kila siku, hata wahenga walisema "Tenda wemu lakini usingoje shukrani".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…