Nsabhi
JF-Expert Member
- Feb 23, 2011
- 1,093
- 162
Ndugu wanaJF naomba kujuzwa hivi PCCB wanafanyeje kazi zao maana kila maovu yanapoibuliwa wao ndo wanajidai kufuatilia. Kwani wao hawana intelligency ya kutosha mpaka waibue wengine kwanza ndo nao waibuke? Nimekuwa na wasiwasi sana juu ya utendaji wa Takukuru. Hivi majuzi kwa mfano baada ya kuibuka kashifa ya vigogo kuficha fedha nje ndo Takukuru ikaibukakwa nini isifuatilie mapema suala hili? Pia suala la kashfa ya baadhi wa wabunge kupokea rushwa liliibuliwa na watu wengine kwanza ndo PCCB ikasema inachunguza. Hivi ndo PCCB inapaswa kufanya kazi naomba wanaJF mnijuze.