Hivi pccb wanafanyaje kazi zao?

Nsabhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2011
Posts
1,093
Reaction score
162
Ndugu wanaJF naomba kujuzwa hivi PCCB wanafanyeje kazi zao maana kila maovu yanapoibuliwa wao ndo wanajidai kufuatilia. Kwani wao hawana intelligency ya kutosha mpaka waibue wengine kwanza ndo nao waibuke? Nimekuwa na wasiwasi sana juu ya utendaji wa Takukuru. Hivi majuzi kwa mfano baada ya kuibuka kashifa ya vigogo kuficha fedha nje ndo Takukuru ikaibukakwa nini isifuatilie mapema suala hili? Pia suala la kashfa ya baadhi wa wabunge kupokea rushwa liliibuliwa na watu wengine kwanza ndo PCCB ikasema inachunguza. Hivi ndo PCCB inapaswa kufanya kazi naomba wanaJF mnijuze.
 
Kawaulize. Wewe unakaa wapi Tanzania hii kusiko na ofisi yao?
 

Ili uelewe vizuri fanya ubadhilifu wa mali ya umma,najua watakufuata tu halafu hapo ndo darasa lako lihusulo namna ya ufanyaji kazi wa pccb litaanza.
 
hata mi najiuliza, maana rushwa inaliwa hadharani kabisa.
Mi mwenyewe nimekoswakoswa na afisa mmoja wa ardhi.
 
Hawafanyi kazi bali wanafanya usanii huku wakilipwa ujira na marupurupu mazuri, vinginevyo rushwa isingeshamiri kiasi hicho hadi kuingia mjengoni.
 
hata mi najiuliza, maana rushwa inaliwa hadharani kabisa.
Mi mwenyewe nimekoswakoswa na afisa mmoja wa ardhi.

Kama inaliwa hadharani, wewe mwenyewe umechukua hatua gani? Maafisa wa pccb hawawezi kuwa kila mahali kwa wakati moja. Watajuaje bila kuambiwa? Watashindaje kesi bila ushahidi kutoka kwako? Angalau ungewakemea wala rushwa, wangeinama, wangeona aibu na kuacha kula rushwa. Wananchi wa kawaida tuwe na hasira na wala rushwa, wataacha bitendo vya rushwa. Tusiwaachie pccb peke yao, hawataweza.
 
Hawa jamaa kama huna pesa hawakufanyii kazi ila kama hauna kitu lazima mkutane cortini maana kuna jamaa yangu huko singida aliomba rushwa ya buku4 amekula miaka3 au fayn laki5 ila kuna jamaa yangu mwingine alipigaga vijicent mpaka leo anapeta,

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…