Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari,Maana ananiambia Mara ya mwisho kwenda alipima presha ilikua 114/98
Leo kaenda eti ipo 93/58
Wamempa tu vidonge vya kutafuna, vipi iyo hali sio hatari kwa afya ya mama na mtoto?
Ujauzito ni wa kwanza,Habari,
Kabla ya yote, ni muhimu kuelewa kuwa, suala la presha wakati wowote na pia kipindi cha ujauzito si suala la namba pekee. Wakati wa ujauzito pia huzingatia kiasi cha mabadiliko ya presha kabla na baada ya mama kuwa mjamzito. Hapa, namba pekee hazisaidii sana.
Hivyo, presha ya juu huwa ni kawaida kwa kuwa chini ya 139/89 mmHg na mabadiliko ya kupanda yasiyozidi 30/15 mmHg ndani ya muda wa ujauzito.
Pia, presha si suala la kuwa na namba moja bali kuwa ndani ya uwiano. Ingawa kuna watu wana presha chini ya kiwango na hiyo ni sawa kwao.
Presha pia huweza kuathiriwa na hali ya mtu ndani ya muda mfupi na baadaye kurejea sawa. Presha huweza kuathiriwa na saikolojia, vinywaji na pia stress yoyote kwa mwili (physical vs saikolojia). Hili hufanya presha kuwa si kitu cha kufikia mwafaka kwa kupima mara moja tu. Isipokuwa kwa zile zilizo mbali sana, mfano: 220/120 mmHg.
Hivyo, ni vyema kuzingatia hayo kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya hali ya PRESHA.
KWA MGONJWA:
1: Presha (114/98)mHg, ilipimwa mara ngapi kabla ya kufanya maamzi ya mwisho kuwa iko juu? Hapa namaanisha ndani ya hudhurio moja/siku moja vs siku tofauti pia).
2: Dawa anatumia?
3: Vidonge alivyopewa vinaitwaje?
3: Kiasi gani (mg) vs vingapi? Vs mara ngapi kwa siku?
4: Alifanyiwa vipimo vingine vyovyote?
5: Upimaji wa presha ni vizuri kuandamana na mwenendo wa kiasi cha mapigo ya moyo ili kutoa picha halisi.
6: Mgonjwa kwa sasa ana malalamiko gani?
7: Presha ya pili (93/58)mmHg, ilipimwa mara ngapi ili kujiridhisha?
8: Ujauzito wa ngapi? Kuna historia husika huko nyuma?
NB: YOTE HAPO JUU NI YA KITAALAMU, HIVYO USHAURI WANGU NI KUPATA MTAALAMU WA KUPITIA MCHAKATO HUO HUKU AKIWA AMEMUONA MGONJWA NA PIA KUMFANYIA UCHUNGUZI YAKINIFU. MAAMZI YOYOTE BILA HIVYO SI YENYE AFYA NJEMA SANA. ILA NI MUHIMU MGONJWA HUYU ATATHMINIWE VIZURI.
Ujauzito ni wa kwanza,
Kipimo cha Mara ya kwanza kilipimwa Mara moja tu, kipimo cha Jana nacho kimepimwa Mara moja tu, dawa alizo pewa, zinaitwa AGOFER,
Afu kuhusu malalamiko hana hata shida yoyote yupo vizuri kabisa, ila alivo pewa izo dawa za kutafuna ndo akajiskia vibaya hadi kutapika,
Sawa mtalaam asanteAgofer ni kwa ajili ya madini chuma na folic acid. Kwaajili ya kuhakikisha mama anakuwa na damu ya kutosha na pia ustawi mzuri wao wote wawili.
Unahitajika mwendelezo wa ufuatiliaji wa presha yake kama ilivyo kawaida.