Uchaguzi 2020 Hivi Rais anajua uongozi wake na uzima wake unatokana na jasho la Watanzania wote?

Uchaguzi 2020 Hivi Rais anajua uongozi wake na uzima wake unatokana na jasho la Watanzania wote?

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Kwa hakika kama sio DHARAU basi ni KIBURI. Kama sio hivyo viwili, basi ni KUJISAHAU. Na kama sio vyote labda ni Mzoefu wa KUTELEZA ULIMI.

Serikali yoyote inafanya kazi sake kwa kodi toka kwa wananchi wake. Bila kujali kabila, dini, msimamo wa kisiasa, jinsia nakadhalika.

Nimekuwa nikisikitishwa sana kauli za Ndugu Magufuli kuwa eti, serikali yake inashinndwa kupeleka maendeleo katika baadhi ya maeneo kisa eti, yamechagua vyama vya upinzani!

Mheshimiwa Rais ina maana maeneo haya hayalipi kodi serikalini? Au wewe pesa ya kupeleka maenndeleo huko Kwingine huwa unatoa wapi?

Kwa kweli kauli hii ni dhihaka kwa watu wako, na kuwageuza watu wengine kama wapuuzi tu ndani ya nchi yao.

Napenda tu Magufuli ajue, anakula, anaishi vizuri, analindwa na anatunzwa ki VIP kwa kodi ya watu wote wanaoipenda CCM na vyama vyingine vya UPINZANI.

Kwa kauli hizi, Mimi mlipa kodi wa UPINZANI nitakuwa na haki ya kukushtaki Duniani na Ahera.

Ni aibu kauli kama hiyo kutolewa na kiongozi, anayepaswa kuwa RAIA na MZALENDO namba moja wa Nchi.
 
Sidhani kama analifahamu hili maana yeye anajiona ni rais wa ccm tu wengine ni wakimbizi ndani ya nchi hii,wenye hati miliki ni kijani tu,ngoja upepo ubadilike nashuhudia wengi wakienda ukimbizini
 
Sidhani kama analifahamu hili maana yeye anajiona ni rais wa ccm tu wengine ni wakimbizi ndani ya nchi hii,wenye hati miliki ni kijani tu,ngoja upepo ubadilike nashuhudia wengi wakienda ukimbizini
Haendi mtu ukimbizini,tutabanana hapahapa
 
Yeye hapeleki maendeleo kwa wapinzani lakini kodi anakusanya bila kujali itikadi za chama
 
Imekuwa bahati mbaya kabisa kuwa na kiongozi wa hovyo namna hii nchi hii tumpige chini mwisho wa mwezi huu!
 
Sidhani kama analifahamu hili maana yeye anajiona ni rais wa ccm tu wengine ni wakimbizi ndani ya nchi hii,wenye hati miliki ni kijani tu,ngoja upepo ubadilike nashuhudia wengi wakienda ukimbizini
Aliwafukuza nchini?
 
Back
Top Bottom