Hivi Rama Dee aliwakosea nini watanzania

Duh! I'm I living under the rock or something? Kwa muda wote wa maisha yangu nimeishi na kufuatilia mziki wa hapa Tanzania na sijawahi kusikia kazi nzuri za huyu jamaa? Ila nakiri hii ngoma ni miongoni mwa nyimbo Kali kuwahi kusikia kwamba ni mali ya mmatumbi i mean mswahili. Nilikuwaga naamini Nurueli ndo mkali pekee wa RnB ninaemjua..hapana kumbe huyu dogo nae wamo.

Perfect voice with an amazing vocal techniques.. He made lugha yetu ya kiswahili ionekane smooth and sentimental.

Life is not fair and has never been fair kwa kweli..Diamond na Vanessa wanakwapua tu matuzo kimataifa ilhali Rama dee yuko kibanda umiza pale Manzese anajipoza na EPL.

Kiukweli huyu jamaa levo zake ni akina John legend au Joe Thomasi.

Ni sawa sawa na Lokua Kanza mwanamuziki toka Congo jamaa ni well talented and gifted lakini hapewi respect kihivyo wala hapati pesa za kutosha kutoka kwenye kipawa chake cha muziki. Its sad! Ukisikiliza ngoma zake kama "Mutoto" au "Nakozonga" au "si tu pars" pamoja na "kwetu mbali" ndo utajua jamaa anastahili heshima ya ulegendary. Ni papa wemba pekee ndo anakiri umahiri wa huyu jamaa na kulalamika wacongoman kutomconsider jamaa kama nguli wa fani ya muziki.
 
HUYU MCHAGA ANAJUA SANA KUIMBA MBONA GOMA LINAPGWA SANA TVE NA EA RADIO SANA TU
 
One of the best musician in Tanzania ni huyo jamaa.Music wake mzuri sana
 
wote wanaomsifia rama dee ni mashabiki wenza wa alikiba!!

najua nimewakwaza ila nawaona tu....mnakula ubuyuuuu....
 
Huyu jamaa anajua huo wimbo ni shida. Changanya nyimbo za ben pol hazioni ndani kwa kipenda roho.
Ila ndiyo hivyo watz wengi kama hawaoni na wengine hawamjui.
Hapo ndipo ujue mziki ni zaidi ya kuwa mwimbaji mzuri.
Sangoma anahusika kwa sana kibongobongo
 
Kifupi Rama dee anaishiAustralia na anafanya shughuli zake huko.Jamaa hazipi promo nyimbo zake ni kama ame relax baada ya kwenda Australia.Kwa wanaofuatilia muziki Rama Dee sio jina geni alishafanya ngoma na Prof Jay J.O.S.E.P.H aliimba chorus. Kwa miaka ile msanii mchanga kufanya ngoma na Niga Jay ilikua sio mchezo.Jay alikiona kipaji cha Rama Dee.Kuna ngoma ya Nikki wa Pili Good life Rama Dee kaitendea haki sana KWENYE Chorus.
Jamaa ana album kabisa ambayo aliitengenezea kwa Amba Iringa.Amba alikua anamkubali sana jamaa alikua anajigharamia nauli tu ya kufika Iringa, kula ,kulala na kurekod ilikua bure kwa Amba.Kifup jamaa ana talent kasikilize ngoma hizi Kikao cha Family,Sara,sio waoaji hao,naachana nao,najua,mazoea,kuwa na subira,usihofie wachaga n.k n.k.
Ni kweli Rama D ndiye aliyempokea Joh Makin na akaishi naye kwao lakini jamaa alipata tu dem mzungu ni kama career yake kibongobongo imepotea na mziki imekua kama leisure tu kwake na sio kazi.Leo hii Johyupo mbali sana kimzimki kuliko hata wale waliomsaidia hii ni kutokana na nidhamu ,heshima na kuishi na watu vizuri,Nakiri bifu ya vinega ndo ilimpoteza Rama Dee kwenye muziki.Naamini Rama Dee akiamua kurudi kwenye game na kuwekeza haswa kwa promo na media tour atafika mbali.Uliza watu wa Iringa kupitia Ebony Fm wanamnjua sana huyu mtu.
 
Tatizo jamaa ana mambo ya kike na ndio yamesababisha apotee kwenye game,aliingilia ugomvi wa Ruge na sugu sasa walivyo kuja kupatana yeye akabaki yupo yupo na ngoma zake cloud hawazigongi!
Acha wivu Mkuu! Rama D ni zaidi ya Mbongo fleva....! So utasema kina Vinega wana mambo ya kike? Wewe niaje babu? Wewe wa kike au wa kiume?
 
Nataka kumfahamu ruge na clouds yake,nasikia hata bint machozi alikuwa anaelekea taaban baada ya nyimbo zake kutopigwa.
 
Huyu jamaa kifupi anajua na anaimba mapaka msikilizaji unasema kweli jamaa ni bonge la rnb killer ...
Au huyu jamaa haishi bongo?
 
Jiwe walilolikataa waashi limekuwa Jiwe Kuu LA pembeni.
Muda utafika, muda utaongea, muda utaponya majeraha yote ya mkali Rama Dee
 
Kiukweli jamaa anajua sana kuimba na tungo zake zimesimama vibaya sana...ila nadhan ana ulimbukeni wa kuleta harakati kwenye muziki...

in short, ana kipaji ila hana akili ya kutoka kimuziki na kimasoko...sijui kakulia bush gani huyu jamaa.
Bush LA Australia ndio anaishi
 
Ila jamaa hata kabla ya antivirus hakuwa na jina kivile, yaani nyota yake haijawahi kung'aa pamoja na ukali wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…