Hivi rasimu ya Jaji Warioba inaweza kupitishwa kuwa Katiba mpya kama ilivyo?

Hivi rasimu ya Jaji Warioba inaweza kupitishwa kuwa Katiba mpya kama ilivyo?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naona wadau wengi wa Katiba mpya wanaipigia chapuo Rasimu ya Jaji Warioba

Ndio najiuliza kwanini huyo Rasimu isipitishwe tu kuwa Katiba mpya?

Maana Kikosi kazi cha Prof Mkandalla na zitto kabwe wadau hawakifatilii Kabisa
 
Sidhani kama CCM mtakubali maslahi yenu kuwekwa hatarini, mchakato wa KM ni wa watanzania lakini nyie mmeugeuza kuwa interest ya chama chenu.
 
MKUU

Rasimu ya Warioba inatosha kabisa Kuwa Katiba mpya!

Kuna marekebisho tu idadi ya serikali ndio kuna mvutano lakini imeshaamriwa zibaki Mbili kama zilivyo kutokana na utafiti wa mashirika ya kijasusi!!(refer uzi wa Tumia akili wa majuzi) tu!!

Nakuomba tuendelee kusisitiza ule wimbo wetu ule;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe Katiba mpya""!!
 
Naona wadau wengi wa Katiba mpya wanaipigia chapuo Rasimu ya Jaji Warioba

Ndio najiuliza kwanini huyo Rasimu isipitishwe tu kuwa Katiba mpya?

Maana Kikosi kazi cha Prof Mkandalla na zitto kabwe wadau hawakifatilii Kabisa
RASIMU alosimamia Judge Warioba irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Mzee wetu arudishwe kwenye Tume AAPISHWE, mukandala arudi kufundisha.

Tutaenda Kwa tahadhari kubwa kwenye hatua zinazofuata kwenda kwenye Bunge la KATIBA.

Tupate mjadala mpana, tuondoe uchama na maslah binafsi,

Sheria kandamizi ziondolewe zenye kupendelea chama kimoja.

Makundi yote muhimu ya Machinga,vyama vya siasa, wakulima, wafanyakazi, Bodaboda, wafugaji, wafanyabiashara, asasi binafsi, wanafunzi, nk wapewe fursa sawa kuingia BUNGE la KATIBA.

Hatimaye tupate KATIBA Bora itayodumu zaidi ya miaka 400 bila viraka.

Ameeeeen.
 
Naona wadau wengi wa Katiba mpya wanaipigia chapuo Rasimu ya Jaji Warioba

Ndio najiuliza kwanini huyo Rasimu isipitishwe tu kuwa Katiba mpya?

Maana Kikosi kazi cha Prof Mkandalla na zitto kabwe wadau hawakifatilii Kabisa
Maoni ya Wananchi wenye nchi yalikusanywa na chombo chao-Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Jaji Warioba.Hayo maoni yanayokusanywa sasa hayawezi kuwa mbadala wa yale tuliyoyatoa kipindi kile!
 
Ile katiba si nzuri maana kuna sehemu inaongelea 50/50
Hii itasababisha watu dhaifu waingie bungeni sababu hata kama mtu kateuliwa na chama na uwezo wake mdogo bado atapita

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Unaongelea KATIBA PENDEKEZWA au RASIMU kabla ya uchakachuzi,?
 
Back
Top Bottom