Naona wadau wengi wa Katiba mpya wanaipigia chapuo Rasimu ya Jaji Warioba
Ndio najiuliza kwanini huyo Rasimu isipitishwe tu kuwa Katiba mpya?
Maana Kikosi kazi cha Prof Mkandalla na zitto kabwe wadau hawakifatilii Kabisa
RASIMU alosimamia Judge Warioba irudi mezani mjadala uanzie hapo.
Mzee wetu arudishwe kwenye Tume AAPISHWE, mukandala arudi kufundisha.
Tutaenda Kwa tahadhari kubwa kwenye hatua zinazofuata kwenda kwenye Bunge la KATIBA.
Tupate mjadala mpana, tuondoe uchama na maslah binafsi,
Sheria kandamizi ziondolewe zenye kupendelea chama kimoja.
Makundi yote muhimu ya Machinga,vyama vya siasa, wakulima, wafanyakazi, Bodaboda, wafugaji, wafanyabiashara, asasi binafsi, wanafunzi, nk wapewe fursa sawa kuingia BUNGE la KATIBA.
Hatimaye tupate KATIBA Bora itayodumu zaidi ya miaka 400 bila viraka.
Ameeeeen.