Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 262
- 361
Hellow JF.
Hivi sasa jamii zetu zinapitia wakati mgumu sana katika swala la malezi na makuzi ya watoto ukilinganisha na jamii za miaka ya yuma.
Hivi leo kumekuwa na visa vingi sana mitaani vikahusishwa na malezi pamoja na makuzi ya watoto.
Leo jamii zinalia juu ya tabia na mienendo ya watoto wao, wengi wamekuwa na tabia zisizofaa, wengine wamejiingiza katika ubakaji, wengine kujiuza kama ambavyo samaki huwa zinauzwa sokoni, wengine wamejigeuza jinsi zao, wengine wamegeuka mashoga na wasagaji, wengine wanatembea na watu umri wa wazazi wao na bado hawaoni shida yoyote. Jamii imejielekeza zaidi katika kuangalia maisha yao ya sasa kuliko maisha ya vizazi vyao kwa karne nyingi zijazo.
Sasa basi turudi kwenye mada, kumekuwepo kwa wimbi ka kesi na migogoro mikubwa baina ya familia moja na familia nyingine. Na sehemu kubwa sana migogoro hiyo imesababishwa na watoto.
Wazazi wamekuwa hawana desturi nzuri ya kuwasimamia watoto wao ili wakue katika utaratibu mzuri ambao utawawezesha kuishi vizuri na jamii inayomzunguka pamoja na kutii sheria za eneo husika na nchi kwa ujumla, sasa wazazi wanapofeli katika jukumu hili la msingi sana hupelekea watoto kuishi maisha ambayo sahihi na mwisho wa siku mtoto anaishi akijilea mwenyewe katika njia zake ambazo kimsingi zinamapungufu makubwa sana.
Mfano 1. Leo ni kawaida sana kukutana na mtoto mdogo njiani na asikusalimie na asiwaze wala nini. Lakini nyote ni mashahidi enzi zetu miaka ya 70-90 ilikuwa ni kosa la jinai mtoto kutoheshimu watu wazima kwa namna yoyote ile. Na kipindi hicho kila mtu alikuwa na wajibu kwa mtoto hatakama sio mtoto wake wa kuzaaa.
Mfano 2, unaweza kukutana binti/kijana wa kiume katika maeneo fulani na asikuogope wala nini na ukicheza anaweza hata kukudhalilisha, hii ni alama kwamba mambo sio mambo.
Sasa ni kwa namna gani watoto huwagombanisha wazazi/walezi, ni kwa namna hii:-
1. Kwakua wazazi wenyewe ndio ivo hawana misingi mizuri ya kuwalea vyema watoto, mtoto anakuwa ameshakengeuka tokea kwao na hivyo hujikuta anafanya matendo ya hovyo kwa mtoto mwingine ambae matharani wazazi wake wamemlea katika utaratibu mzuri, hali hii hupelekea wazazi wa pande zote kusigana na kutengeneza mgogoro mwingine mkubwa saana ambao mwisho wa siku hupelekea uhasama na visasi vya kudumu baina ya familia izi.
Matokeo ya haya ni kwamba wazazi wa pande zote mbili wanatafuta ushindi wa kesi, kunyenyekewa, kuonekana wao sio wakosaji kama wazazi.
Wanasahau kabisa jukumu lao la msingi juu ya watoto ambao ni kuwalea katika mazingira mazuri yatayopelekea mafanikio makubwa ya watoto wao kwa siku za hapo usoni.
Ujumbe kwenu wazazi.
1. Tujitahidi sana kusimamia kwa karibu maadili na tabia ya jumla ya watoto wetu.
2. Simamia kikamilifu mahitaji ya mtoto kulingana na mazingira, maan matunzo ya mtoto sio tu kumlisha na kumvalisha.
3. Acha kutafuta ushindi usio na msingi wowote badala yake tumia nguvu hizo kumrekebisha mwanao kwenye maeneo ambayo ana madhaifu.
4. Acha kabisa kuendeleza magomvi yanayosababishwa na mtoto wako kwa namna yoyote badala yake kemea kwa nguvu zote.
5. Usipuuze kabisa kumpiga/kumfundisha adabu mwanao anapokosea.
6. Acha kulea watoto kizungu tambua wewe ni mwafrika, mwanao ni mwafrika, na mnaishi afrika. Kwaiyo acha kupumbazwa na maisha ya tamthilia.
Mwisho kabisa , karibu kwa mawazo, nyongeza ili tujifunze kwa pamoja.

@KIRAKA