KERO Hivi serikali haiwaoni hawa wanawake wanaocheza Ngoma za Uchi maarufu kama Baikoko?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Watendaji wa kata so ni sehemu ya serikali?maadili ya nchi ni mambo binafsi tangu lini?
 
Miaka 14 nyuma nilikuwa nikistaajab kuona waafrika Magaribi wakicheza/kutingisha matako nusu uchi kwenye makusanyiko yao (Sabar /Mapouka Dance) nikawanajisemea wana laana hawa watu, hiki kikombe kitupitie mbali.
Ila sasa upepo umebadilika Wadada na wamama wa Tanzania sasa wanaocheza uchi wa mnyama mbele ya watoto huko mitaani. Iwe vanga,Kigoma cha Shetani au Brassband lazima wavuenguo kama wendawazimu, huko nje(Mitandaoni) wanasema eti ndio utamaduni wetu tokea zamani.
Maadili hayapo tena huko kwenye kumbi ni Usodoma mtupu wanaingiliana kama wanyama na video zinauzwa dunia Naima, Baikoko inavuma sio Mapouka tena.
 
Hovyo sana yani,tena kunanyimbo za singeli za hovyo zinaimba nataka kwenda toilet,mara mi msela mavi ujuwe nitakutoboa na bisibisi ujuwe yani hovyo.
 
Hao watendaji wenyewe kipindi kile cha kampeni za uchaguzi serikali za mitaa walikuwa wanasindikizwa na hivyo vigoma vya shetani.
 
Kumekua na Tabia, ambayo inaonekana kuzidi kushamiri, huku mamlaka zikiwa zimebaki kimya bila ya kuchukua hatua yoyote,

Mchezo wa baikoko unazidi kushamiri na unahusisha kucheza uchi, kufanya mapenzi hadharani, wakati mwingine mchana kweupe , na watoto wakiwa wanaangalia, Maeneo ya uswahilini hasa Buza, Mbagala, Manzese inaonekana kama tamaduni Za kawaida.

Ningeomba Serikali iangalie hii Tabia na kuichukulia hatua, kwani inaharibu utamaduni na ustaarabu wa jamii, pia kurudisha nyuma jitihada za kupambana na Tabia hatarishi, magonjwa ya zinaa na Afya ya jamii hasa watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…