Hivi serikali haiwezi kuhalalisha bangi "for exportation only"?

Hivi serikali haiwezi kuhalalisha bangi "for exportation only"?

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
Dah!

Kuna habari nimeiona BBC inaongelea kuhusu uhitaji wa bangi kwenye nchi za wenzetu kwa matumizi ya dawa nikahuzunika!
Watu wanaohitaji hii kitu ni wengi, Demand ni kubwa kuliko supply na hela wanatoa kupata kimsokoto ni kubwa sana. Which is a benefit for the farmers! Kwanini hatuioni hii kama fursa?

Kuna watu wanateseka na dawa tunayo. Ajabu ni kuwa, askari wetu, kila iitwayo leo wanaiteketeza bila kujali.

Ripoti mbali mbali zinaonyesha mmea huu (marijuana) hauna madhara yeyote kwa mtumiaji KAMA hatochanganya na vileo vingine na unaweza kutumika kama dawa!

Kinachonishangaza serikali yetu, Tanzania, imekomaa na msimamo wa kuwa bangi ina madhara! Madhara yapi ikilimwa kwaajili ya matumizi ya kibiashara?? Italeta Mapato lakini pia ajira. Madhara yapo wapi hapo?

Nimeona wabunge wawili wakipigania ihalalishwe ila serikali ikakataa. Last time, it was afande. Shida ni kwamba alisema point nzuri ila aliiua kwa maelezo yake.

Kuuliza sio ujinga. Naomba kujua kama haiwezekani kukawa na utaratibu f'lani - Wakahalalisha kulima huu mmea kwa ajili ya biashara baadala ya matumizi ya kivuta kwa nchi yetu, Yaani watu wakalima tu kwaajili ya exportation tu!

Najua kutakuwa na wabishi wachache, maana mTanzania ukimwonjesha asali kwa kumruhusu alambe mkono wako, anaweza kuukata akakimbia. Lakini binafsi, naona faida zitakuwa nyingi kuliko hasara, au?
 
Hivi sababu hasa ya kuzuia bangi ni nini?

kama unaruhusu sigara na pombe kwanini uzuie bangi? kwan nchi ambazo wameruhudu bangi kuna madhara yoyote wamepata mpaka sada?
 
Uta- export vipi bila kufanya sampling na kuangalia quality, unaweza kuuza supu bila kuonja chumvi?
 
Bangi ina medicinal uses, ila kutumia kwake kama dawa sio kwa kuivuta, watu wanachokiogopa ukiruhusu medicinal purposes watu wata-abuse hio privilege na kuitumia ndivyo siyo.

Nchi hii yenye watu wenye shida hawana kazi, wanajaribu kila kitu (viroba, petroli n.k.) ukiwapa opium ili wajiliwaze baada ya kushindwa kwenye betting na kupigwa na maisha ni recipe for disaster majanga yake kwakweli yatakuwa maradufu kuliko faida.

Bora wakishindwa kabisa wasiikataze ILA WASIRUHUSU, yaani wakiamua wakiona legally ume-abuse wanaweza kukushitaki sheria (kama dada poa hata kama wanajua wapo katika madanguro ila hawawashiki sana mpaka wakizidi)
 
uta- export vipi bila kufanya sampling na kuangalia quality, unaweza kuuza supu bila kuonja chumvi?
Am literally not sure how this is going to be possible. But am certain someone in here will give us clear answers!
Tuvute subra, Mkuu. Ukisoma heading yangu sina conclusion. Mimi pia nipo njia panda!
 
Am literally not sure how this is going to be possible. But am certain someone in here will give us clear answers!
Tuvute subra, Mkuu. Ukisoma heading yangu sina conclusion. Mimi pia nipo njia panda!
Ofcourse unaweza ukasema hauruhusiwi kutumia bali unaweza kuuza nje. UK sehemu nyingi hauruhusiwi kuuza ila ukishikwa na bangi kidogo for personal use police anaweza akakuachia asikushike.

Tatizo ukishafungua this can of worms ni vigumu sana kuwalimit watu, sababu huyo anayelima ili auze nje atauza na ndani, na walimaji watakuwa wengi na si walimaji tu, bali walimaji watumiaji, na kama nilivyosema taifa lenye matatizo kama hili mwisho wa siku kuleta hizi loopholes ni kutaka mtaa mzima na vijana wote masaa yote wawe Haile.
 
Tatizo lipo kwa watu sasa.

Naomba nitoe mawazo yangu, What if they pick an area ambapo ni ngumu watu wa kawaida kufika. Huko wakawekwa watu maalumu kusimamia na kulima mazao haya! Itakua ni ajira na mapato lakini nahisi pia kwa namna moja tutakuwa tumethubutu ku-balance a somewhat kind of equilibrium.
 
Pia Morally nadhani ni tatizo..

Afghanistan mmea wa cocaine unalimwa sana huko, sidhani kama taifa likiona madhara linayosababisha linaweza kujivunia.., (after all utu inabidi utangulie kabla ya material things).., ingawa bangi ndio inaweza kulimwa kama dawa na ni dawa.., ila kuilima kwa kiasi kikubwa sana na kusifika kama top producer wa bangi.., kuna uwezekano wa kujikuta tuna-supply watu wapate sigara kubwa..

Njia nyingine kuna nchi bangi inauzwa pharmacy kama mtu ana uhitaji anaweza kununua huko kwa prescriptions...
 
Pia Morally Afghanistan ndio mmea wa cocaine unalimwa sana huko, sidhani kama taifa likiona madhara linayosababisha linaweza kujivunia.., (after all utu inabidi utangulie kabla ya material things).., ingawa bangi ndio inaweza kulimwa kama dawa na ni dawa.., ila kuilima kwa kiasi kikubwa sana na kusifika kama top producer wa bangi.., kuna uwezekano wa kujikuta tuna-supply watu wapate sigara kubwa..
Njia nyingine kuna nchi bangi inauzwa pharmacy kama mtu ana uhitaji anaweza kununua huko kwa prescriptions...
Upo sawa kabisa. Twende tu, labda muda ukifika itawezekana.!
 
Bunge la Ndugai hili lililosheheni mambumbumbu liko bize kutengeneza sheria za kishenzi na kibabaishaji!
 
Kuna wamarekani wanakamua na ku-pack Kisha wana-export mafuta ya mbegu za bangi duniani kote kwa ajili ya wenye Peripheral Neuropathy na wanapiga pesa tu.
 
Kuna wamarekani wanakamua na ku-pack Kisha wana-export mafuta ya mbegu za bangi duniani kote kwa ajili ya wenye Peripheral Neuropathy na wanapiga pesa tu.
Inabidi serikali ifanye namna bhana.
 
Duh!! Ila wangeruhusu tu ila itumike Kama tiba
 
Back
Top Bottom