Hivi Serikali ipo serious kupambana na Delta variant (Corona 3)?

Hivi Serikali ipo serious kupambana na Delta variant (Corona 3)?

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Hivi Serikali yetu ipo serious kupambana na ugonjwa wa Delta (Indian variant)yaani corona 3?

Wenzetu,ndugu zetu Waganda,DRC,Rwanda Serikali zao zimechukua hatua kali na madhubuti kukabiliana na huu ugonjwa hatari.

SINA HAJA YA KUANDIKA MENGI,WENZETU WAAFRIKA WANATEKETEA HASA UGANDA NA WANAISHI NA KUABUDU KATIKA SAYARI HII HII TULIYOMO SIE WATANZANIA.

Baadhi ya mifano ya kuzembea inayofanywa na serikali kwa uchungu nadiriki kutaja baadhi .

1)Kuruhusu watazamaji elfu 60 kuingia kesho kuangalia mechi kati ya Simba na Yanga.mkusanyiko huu ni mkubwa sana ambao unaweza kutuletea madhara makubwa.

2)Kuruhusu abiria kujazana kwenye Daladala.

3)Kutangaza mitandaoni,magazetini,redioni,Kwenye televisheni namna ya kujikinga na ugonjwa huu.

4)Kupiga marufuku mikusanyiko yote ya watu zikiwemo sehemu za ibada za dini zote.

ATHARI ZA UGONJWA HUU ZIKIANZA KUSAMBAA NA KULETA MADHARA, HAWAHAWA WENYE TAMAA YA KUINGIZA MAPATO WATAKUA WA KWANZA KUISHUTUMU SERIKALI YAO.TUJIKINGE SASA.

Mwisho kama Watanzania tutambue kuwa wenzetu hawakuomba kuteseka ila ni kudra ya MOLA,Na sisi tuzidi kuomba huku TUKIJIKINGA.SERIKALI IWEKE ADHABU KALI KWA WANAOKIUKA MIONGOZO INAYOTOLEWA NA WATAALAM WETU.IMEZOELEKA TANGIA AWAMU YA 5 MPAKA RAIS AU WAZIRI MKUU ATANGAZE LAKINI AKITANGAZA MTAALAAM AU WAZIRI TUNADHARAU.

TIME WILL TELL.
 
Let's wait & see what will happen;this is just wave3,there is still wave4,wave5,wave6,wave7,wave+++++++++ waiting for you
 
Achana na madelta hayo watanzania tulishaomba na kufunga. ..tunaamini Mungu anatulinda na ataendelea kutulinda daima. ..tusichoke kuomba
 
These waves go to what number. ..or infinity
 
Jomba acha woga wa kitoto. Tanzania hata hiyo wave 2 hatujaiona. .usitutishe Jomba. .omba kwa anayekupa pumzi kila siku unaamka. ..au unadhani pumzi unazovuta umejitengenezea mwenyewe
 
Kwani Mama SASHA alivyosema "Tunaenda sawa na Ulimwengu unavyoenda kwenye kujikinga wimbi la 3".

Hukuielewa hii kauli???
 
Tupo tupo tu, wenye zao bahati watabaki wasio nazo wataondoka kama zilivyopita zile phase mbili za mwanzo, bado tunabishana nyungu au chanjo? kama chanjo yetu au ya mzungu?
 
Haya mambo ya Delta sijui wimbi la tatu sijui tuseme season ya tatu ya corona hatujui zitafika ngapi, huko Kenya wanajiandaa na ya nne.

Kama tuki concentrate moja kwa moja na haya mambo tutakuja kuuikuta jua limekuchwa.
 
Mikusanyiko inaendelea kama kawa na daladala zinapiga nyomi, watu wanamshangaa mtu anayevaa barakoa.......ili mradi ni vurugu mechi..
 
piga ny
Tupo tupo tu, wenye zao bahati watabaki wasio nazo wataondoka kama zilivyopita zile phase mbili za mwanzo, bado tunabishana nyungu au chanjo? kama chanjo yetu au ya mzungu?
ungu tu kirusi kinatukoma chenyewe
 
kuwa makini kivyako ndugu, kutisha wengine hiyo marufuku. Nenda uganda/kenya kawe serious huko sisi hatuna huo ugonjwa usikii!
Umemchana huyo fala....aende Uganda akawe serious na lockdown yake anayotaka.
 
Back
Top Bottom