Hivi Serikali Moja chini ya Utawala wa Majimbo haiwezekani???

Hivi Serikali Moja chini ya Utawala wa Majimbo haiwezekani???

Mtanke

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
743
Reaction score
1,839
Naona watu wanahofu na serikali tatu mimi sijajiuliza sana kuhusu hilo lakini kwa nini Jaji Warioba hakupendekeza serikali moja chini ya Utawala wa Majimbo?? Zanzibar tuwe na majimbo mawili Pemba na Unguja na Bara yawepo kama nane hivi. Nafikiri kwa hiyo Muungano utakuwa imara zaidi na wa gharama nafuu usio na manung'uniko. Maoni yangu tu jamani maana tushaoleana ati sie ndugu kabisa.
 
Mtanke mimi nakuunga mkono na wengine walipendekeza hivyo. Lakini kama unavyojua Wazanzibari hawatakubali kwa sababu wanafikiri kuwa wanamezwa na kwao ni tusi kulinganishwa na jimbo. Kwa maoni yangu wote Zanzibar na Tanganyika walishamezana. Pendekezo ili lingesaidia sana kutuondolea migogoro isiyo ya lazima, ingesaidia kutuunganisha pamoja kama taifa, lakini pia ingekuwa njia mbora ya kusimamia raslimali zetu.
 
Zanzibar hawawezi kukubali, mtakuwa mnazidi kuwadidimiza, kuna nafasi zao za ulaji watazikosa. Ukumbuke wao wanadai mamlaka kamili.
 
kama kunakosa alilofanya Mwalimu Nyerere ni hili la kuiacha zanzibar iwe na serkali yake!
 
Back
Top Bottom