Anaehusika na kufungua mashtaka kwa kesi zote za jinai ni DPP lakini kwa vile DPP hana omnipresence power (kuweza kuwepo kila sehemu kwa mara moja) basi akapewa uwezo wa kuwaruhusu watu wengine kufungua na kuendesha mashauri hayo kwa niaba yake..ndio maana sehemu nyingine (hasa wilayani) kesi zinaendeshwa na waendesha mashtaka wa polisi (maarufu kama PP) na ndio hata hao PCCB wanashtaki baada ya kupewa kibali cha kuendesha mashauri hayo...tofauti ya PCCB na polisi ni kuwa PCCB kibali chao ni kwa shauri waliloliombea kibali tu likiisha inabidi waombe kingine wakati PP akipewa instrument anaendelea kuendesha mpaka pale atakapozuiwa..
So generally DPP ndie anaedeal na kesi zote za jinai