Hivi Simba mbona kila kitu kinanaenda taratibu sana, kuna uzembe sehemu gani?

G4rpolitics

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
4,369
Reaction score
5,248
Swala la Kocha mpya tunaenda wiki ya tatu hadi leo ni kimya, na ikumbukwe mwezi ujao tuna mchezo wa kimataifa.

Tuweke hilo pembeni, hivi swala la Mkude baada ya wiki 3, ndo linafika leo kwa mwenyekiti wa kamati ya Nidhamu. Tulikuwa tunasubiri nini muda wote huo? hili ni swala kweli la kuchukua mwezi, kujadili Nidhamu ya mchezaji? Tukiachilia mbali swala la Kocha ambalo nalo hadi sasa hata Kocha msaidizi hayupo.

Nimalize Kwa kusema tunamsaka Kocha mpya Kwa sasa, hicho kikosi kinachosajiliwa ni pendekezo la huyo Kocha ajaye au ndo ule msemo apende asipende lazima awatumie hao ambao si pendekezo lake?

Ni kweli hadi Sven anaondoka uongozi haukuwa na taarifa ya kuondoka kwake na kumwandaa mrithi wake?
 
Wanaesema et mambo yao wanayapeleka kiprofeshino ko we tulia tu mda si mrefu utawaelewa tu.
Ni kwamba kuna sintofahamu ktk uongozi wakati wa kushughulikia kila kitu kwa muda mwafaka.
 
mazoezi yanaanza jumatatu na kocha mpya atakuwepo bunju hivyo kuwa na aman
 
Ni kam vile kuna ombwe la uongozi Simba na ni suala la muda tu tutakuja kuona mambo hadharani. Nikiangalia kwa muda mfupi tu Nkwabi na Senzo wote hao wameondoka Simba halafu uongozi unatoa sababu hazina mashiko kabisa.

Na sasa kwenye usajili ni ingiza huyu, toa yule, jaribu huyu, rudisha tena yule ili mradi tafrani tupu. Kwa haya machache yanayojitokeza hadharani sasa ni dhahiri kuwa kwenye bodi ya Simba kuna tatizo na ile kauli kuwa Simba inaenda kuwa sawa na Al Haly, Zamalek, Orlando Pirates itabaki tu stori tu kama stori nyingine.
 
Tatizo la Simba ni Mo ,Barbra na Mkude....mkude kavuruga kichwa ya Moo baada ya kupiga sound chombo yake.
Mo hana maslaho na Simba ndo maana kamleta Barbara kulinda maslahi ya Mo sio Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…