Hivi sisi ndiyo hatuna kabisa mafuta

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Eti wandugu, nchi yetu ndiyo haina kabisa mafuta au hatujatafuta kwa bidii. Tz ni kubwa kuliko Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi ukiziunganisha. Kenya na Uganda wamepata mafuta.

Sasa maana yake Tz iliyokubwa si kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mafuta. Maana tuko eneo moja, na mafuta mengi nchi hizo yamepatikana kwenye bonde la Ufa, bonde ambalo Tz limepita kwa matawi mawili kabisa.

Hivi tumekosa kabisa mafuta?
Kuna pilika zozote za utafiti wa mafuta zinaendelea?
 
Watu wanatoka kwenye mafuta wewe unataka uturudishe uko
 
Yatakuwepo tu, pengine kwenye maziwa makubwa huko au baharini, si Zanzibar wamesema wao wameyaona upande wao?

Nilisikia China alitaka kulipa madeni yote ya EA countries kama watakubali kumpa umiliki wa ziwa lote la Victoria kwa miaka 200, ila tetesi hizo hazikusema kwanini China analitaka ziwa Victoria.
 
Mafuta yapo tele ni sisi kuna Chalinze,kigoma, zanzibar katavi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…