Hivi sisi wanaume ndiyo tabia zetu??

Cheusi umejifunza nini:couch2:

mengi,ila mojawapo nililojifunza ni jinsi ilivyo rahisi kwa mwanamke mwenye mapenzi ya kweli kuishia kulipwa kwa kutupwa kama karatasi iliyopengewa mafua.so scary but what to do as its not easy kumjua atakayedumu na ww hadi kifo kiwatenganishe au atakayekutupilia mbali baada ya ku-do.lord have mercy
 

Its important that everyday before you go to sleep and when you wake in the morning you pray to you loved ones kusudi asije akaingia kwenye majaribu prayers are so important and when you say your prayers and you believe that god has listen to your prayers trust me you will see miracles happening the only problem with us human beings we are not patient tukiomba tunataka tujibiwe on the spot
 
damn you men wenye tabia ya namna hii, 😛out:go to hell woote mnaonanihii wadada wa watu then mnawapa kibuti
 
Hata ukiwa na hamu ya soda ukiishakunywa na kukata kiu basi ile chupa unaifanyia vioja vingi sana mara utakuta inawekewa mafuta ya taa ndani yake mara mafuta ya kula.


Kuna kupenda na kutaka, kutaka ukipata basi ndio mwisho na ukipenda kila siku utaendelea kutaka. tatizo ni kuwa inategemeana na mwanaume, kuna wanaume wengine ambao sehemu zao za siri ni active zaidi kuliko moyo na ubongo, hao ndio wanakuwa hodari sana wa kutakataka, na hawatosheki tena huwa hata wanajisifu kwa kubadilisha wanawake. Kuna wengine ambao akili zao ziko kichwani wao ni tofauti, ubongo ndio unafanya kazi zaidi na ndio unaoongoza mioyo na sehemu zao za siri, wao at least wanamthamini zaidi msichana na mwanamke na kuchague wa kumoenda na kumataka, tofauti na wae ambao sehemu zao za siri ndio zinaongoza ubongo wao. Wakiona tu viti maalum basi akili imehamia hukohuko.
 
damn you men wenye tabia ya namna hii, 😛out:go to hell woote mnaonanihii wadada wa watu then mnawapa kibuti

ila kuna MIJANAUME ina tabia chafu za kishamba na kilimbukeni jamani yaani,kuna wengine wanaweka loud speaker ukiwapigia,sms zako wanaonesha.akiwa nawe anajifanya anajali na kukupenda yaani ni ma mapretender waliofuzu.
 
ila kuna MIJANAUME ina tabia chafu za kishamba na kilimbukeni jamani yaani,kuna wengine wanaweka loud speaker ukiwapigia,sms zako wanaonesha.akiwa nawe anajifanya anajali na kukupenda yaani ni ma mapretender waliofuzu.

Umenikumbusha kisa kimoja kuna siku nimekaa sehemu nakula nyama choma wakaja jamaa wawili wakaa pembeni yangu wakaanza kusema "Aahhh mbona yule Jane nimeishampitia wala hana ladha yoyote ile nilifikiri yuko fresh kumbe hamna kitu used ile mbaya utafikiri daladala" Niligeuka nikamwangalia mshikaji nikasema duh huyo mwanamke anayeongelewa maskini pole zake angejua
 

umenifurahisha jioni ya leo,unatumia nini?agiza unachotaka nakuja kulipa.
umeongea vyama kabisa ndugu yangu.
 

ni kutokua na akili.
ndo hao bongolander anasema sehemu zao za siri ndizo zinazoongoza ubongo wao-
 
nyama zinatufautiana na ladha inatofautiana ya kidari sio paja
maini yatabaki kuwa maini tu, kama ni ya ndama au ng'ombe mkubwa!!!! na virutubisho vyake ni vile vile sio kwamba kidari kina vitamin K na paja lina vitami Y
 
Ninavyoona mimi ni kwamba mwanaume kama mnyama hana tofauti yoyote na jogoo.Huwa siku zote iko katika nature kusambaza genes zake.Lakini ukweli unabaki palepale kuwa binadamu amepewa akili na utashi ili ayaongoze maisha yake.Sasa kwa wale wanaoshindwa kuongoza matamanio yao ndio hao wanaokuwa na tabia za kumpata mtu na kumuona hafai .Lakini ukweli unabaki palepale kuwa huwezi kuwamaliza wote dunia nzima na kila siku wanazaliwa,ni vyema ukachagua mmoja na kutulia naye.
Ninakumbuka kisa cha jamaa yangu mmoja msukuma aliyeoa na kuleta mke ndani.Siku ya kwanza mwanamke akapika ugali mbichi,jamaa akavumilia na ya pili na ya tatu, jamaa siku hiyo vikamshinda akaufunga ugali kwenye baiskeli na kuupeleka ukweni.Alipofika huko baba mkwe akamwambia mwanangu si umependa?Na kama umependa basi nenda ukafundishe yale unayoona yana mapungufu.Kwa ujumbe huo nami nikajifunza kuwa hata kama umempata mtu ambaye hujaridhika naye katika mambo fulanifulani basi ni vyema ukamfundisha ili awe vile unavyotaka.Watu wameoa machangudoa na wakatulia,na kuna watu wamechukua wake vijijini ambako gari inaonekana msimu wa mavuno tu mwaka mzima na umeme kwao hawajui hata kama upo,wakawaleta mjini wakawafundisha na sasa ni wake bora kabisa.Tusijiendekeze na matamanio yetu huko ni kutafuta ngwengwe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…