Hivi Stars tutajifunza hadi lini?

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Habari wana JF na wanamichezo kwa ujumla,
Nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya timu yetu ya taifa maalufu kama Taifa Stars,naona tunarudi nyuma kwakasi zaidi kuliko kusonga mbele.Sina hakika kama kuna mpango wowote na makakati wa kuifanya timu hii yetu pendwa iweze kututoa kimasomaso waTz wapenda mpira.

Binafsi naona tungepandisha wale Serengeti boys ndo wawe timu ya kwanza twende nao taratibu maana naona tunawapa lawama bure makocha (Mayanga),ila kusema ukweli hata aje Pep Guardiola wachezaji wetu wamekomaa na hawafundishiki.Niliuangalia kwa makini mchezo wetu na Algeria nikagundua wanakosa basics nyingi sana za soka kiasi kwamba tusitegemee lolote kwa miaka ya karibuni
.TFF futeni hilo timu tuwekee vijana watatufikisha mbali
 
TZ hatujui mpira time and again tumedhihirisha Hilo. Hata waende hao Serengeti boys bado hatutoboa. Nashauri tuachane na soka tuwekeze kwenye michezo mingine
 
Mpira ni kipaji suala la kocha ni dogo sana . Kuna baadhi ya nchi zina uchumi mkubwa zimewekeza kwenye mpita wa miguu kuanzia accademy za watoto kila sehemu lakini timu zao za taifa hazitoboi. Lakini kuna nchi nyingine wala hazihitaji aaacademy mavipaji wanazaliwa tuu. Makocha hupata maujiko kutokana na vipaji binafsi vya wachezaji.

Hivi bongo tumelogwa na nani?? kwani mbona tunatumia nguvu nyingi sana kulazimisha soka ambayo sii asili yetu!!! ebo!!! kwanini tusibadilishe gia?? yaani watu wawili tuu Samatta na Msuva watuaminishe akili zetu kuwa sasa tunaweza?? mliangalia Algeria wanacheza kama walikuwa wanacheza na vitoto vyao???

walah!!! Stars walicheza kweli kweli tene mpaka jitihada zoa za mwisho,,,,, ebanaeee!!!! wangeamua kukomaa si wangefungatena zile saba!!! Kila mmoja kajazia , yananguzu kama yanakula kokoto .

Haya ilikuwa ya kirafiki kama ilikuwa ya ushindani!!!! Omera!!!!. Tusimlaumu kocha hata kidogo...tusiwalaumu wachezaji hata kidogo wamecheza mpaka kiwango chao cha mwisho.

Tuhame sasa soka sii issue twnde kwenye riadha au ndondi au unaonaje soka tuwaachie wanawake kama Marekani?????
 
Nawakosoa watoa mada wote...tatizo letu viongozi Wa mpira hawana mapenzi ya dhati na mchezo.....mchezo wa mpira wa miguu unahitaji watoto watukutu"bad boys" lakini hapa kwetu wachezaji wa aina hii wanafukuzwa kwenye timu..Christiano Ronaldo mama yake alienda kumdump kwenye academy baada ya kumshinda..Neymar,Zlatan,Suarez,Diego Costa,Gaza,Maradona list inaendea.Leo hii ukienda mtaani ukatafute"masela" tu wakacheze na Ngorongoro au Serengeti boys utaona maajabu..hawa vijana tuwapende jinsi walivyo tutafika mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…