Hivi Tanzania ina uhusiano wowote na Ureno?

Hivi Tanzania ina uhusiano wowote na Ureno?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
TANZANIA inafahamika saana Portugal kuliko nchi nyingi za Afrika.

Nimecheki video fulani YouTube ya ask Portuguese about Afrika.

Watu walikuwa wanataja nchi wanazo sifahamu kutoka Afrika watu wengi wametaja Tanzania kuliko nchi yeyote kutoka Afrika.

Na ndiyo mara ya kwanza kuona TZ imetajwa na watu wengi toka nianze kucheki video hizi. Kwa hiyo inaonyesha Tz inafahamika saana Portugal.
 
Msumbiji alikuwa koloni la Ureno. Vita vya uhuru wa msumbiji vilianza miaka ya 60 mpaka mwaka 1974 ambapo walifikia makabuliano ya kusitisha vita na kupata uhuru 1975.

Vita hii ilipiganwa na FRELIMO. Vita hii ilipata msaada na uungwaji mkubwa wa Tanzania na hata FRELIMO ilianzishwa Dar es Salaam mwaka 1962 chini ya Eduardo Mondlane. Nadhani pale posta (Garden Avenue) kuna makumbusho ya kuhusu mambo haya ya msumbiji jirani na ubalozi wa Uholanzi.

Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi ambaye alisaidia sana nchi nyingi za kusini mwa Afrika kupata Uhuru ikiwemo Msumbiji. Nadhani pia viongozi wengi wa msumbiji ama wamesoma Tanzania au wamefunzwa siasa Tanzania ndio maana hata raisi wa sasa anaongea kiswahili vizuri.

Pengine wareno wanajua hili hivyo ni rahisi wao kujua jirani ya koloni lao aliesaidia. Na wenzetu huwa wanaheshimu watu majasiri na wanaotoa msaada kwa wahitaji.
 
HUKU NI KUJIPENDEKEZA KAMA KAWAIDA YA WANA CCM......Angola na mozambique lazima zitajwe zaidi na wareno.
 
Waitaje zaidi Tanzania haitupunguzii gharama za maisha au shida zetu.

Kama usingizi umekata kaoshe vyombo
 
Back
Top Bottom