Ugawaji wa Tausi huu Ugawaji wa Tausi, kabla ya Raisi Hajagawa tausi kwa wastaafu, kuna hotel inaitwa JS imeshapatiwa hao Tausi kitambo,
Ni mmiliki nani na nani hasa aliruhusu wato Ikulu?
Britannica
Mkuu Britanicca, acha uchokozi na uchochezi, tausi ni ndege tuu kama ndege wengine wote na wanapatikana mahali pengi.
Kwa bandiko hili, ikiamuliwa kufunguliwa kesi ya uchochezi, jee utaweza kuthibitisha kuwa hao tausi wa JS Hotel pale Chato ni tausi kutoka Ikulu yetu?, unamaanisha kuna mwizi kaingia Ikulu yetu, akawaiba wale tausi wa Nyerere pale Ikulu ambao ni nyara za taifa, akawapeleka huko JS hotel?.
Au anamaanisha miongoni mwa watu wenye access na Ikulu yetu, kuna mtu ni mwizi kaiba tausi wetu ambao ni nyara za serikali, na kuwauza kwa JS hotel ya Chato?.
This is criminal liability, hivyo kama kuna tausi wa nyara za serikali pale JS Hotel, Chato, na police wetu wanasoma JF, waanzishe uchunguzi hapo JS kuchunguza yafuatayo
- Jee ni kweli JS hotel ya Chato kuna tausi?.
- Waliwapata wapi hao tausi?
- Wana vibali vya kumiliki nyara za serikali?
- Kama ni tausi kutoka Ikulu yetu, nani aliruhusu nyara hizo za serikali kuchukuliwa na kupelekwa hotel binafsi?.
- Kama ni kweli tausi hao wa JS hotel ni kutoka Ikulu yetu, then huu nao ni ufisadi tuu kama ufisadi mwingine wowote!.
NB. Angalizo: Kufuatia JS hotel kuwa karibu na Ikulu ya Chato, usikute tausi ambao Mkuu Britanicca amewaona ni tausi wa Ikulu ya Chato wakiranda randa mitaani kama wale Tausi wa Ikulu ya Magogoni wanavyo randa randa maeneo mengi, and this being the case, hakuna kesi wala hakuna issue!
P