Hivi TBS inafanya kazi gani kama Wafanyabiashara wanaingiza 'Bidhaa Fake' na kutangaza waziwazi, iPhone 15 Tsh. 380,000?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Hii nchi ina mambo ya ajabu sana mpaka mtu unashindwa kuelewa hizi taasisi zinafanyje kazi. Mfano mzuri Shirika la Viwango pamoja na Tume ya Kuwalinda Walaji ziko wapi wakati watu wanaingiza Bidhaa Feki kila mahali na wanauza kwa uhuru kabisa. Imagine mtu anatangaza kabisa iPhone 15 Pro ni Tsh. 380,000. Hivi kwa style hiyo si kuna watu wanalipa hadi mamilioni bila kujua wananunua Simu Feki?​


Your browser is not able to display this video.
 
Tanzania ukitaka kununua kitu chochote basi nunua sehemu sahihi. Kama ni simu, nenda maduka yanayofahamika. Achana na hizi chochoro za Kariakoo.
 
Reactions: apk
Ukiwa na akili timamu ukaambiwa simu ni copy alafu ukanunua kwa bei ya juu akili yako pia itakuwa haina akili.
Unless kama zina madhara kiafya hapo ni mwendo wa wajinga ndio waliwao AKA 'Kasongo yeye"
 
Ukiwa na akili timamu ukaambiwa simu ni copy alafu ukanunua kwa bei ya juu akili yako pia itakuwa haina akili.
Unless kama zina madhara kiafya hapo ni mwendo wa wajinga ndio waliwao AKA 'Kasongo yeye"
Mkuu upo sahihi.kabisa Mimi ni.muhanga!
 
Lakini kuna vyombo vinalipwa kuzuia mwananchi masikini asiibiwe kwa nini hawazuii? Unajua mwananchi akiona kwenye tv kuku akaambiwa ni nyumba anaamini kwa kuwa tv imesema? Sasa ndiyo maana Kuna vyombo vya kumlinda. Huu ujinga hata china kwenyewe wakikukamata na vitu bandia wanakunyonga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…