Hivi timu isiyo na kocha haiwezi kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa soka

Hivi timu isiyo na kocha haiwezi kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa soka

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Nimekuwa nikitafakari dhana na umhimu wa makocha hasa katika mchezo wa soka napata mkanganyiko! Huwa najiuliza ingawa kunaweza kuwa na umhimu wa timu kuwa na kocha, je kukosekana kwa kocha timu haiwezi kufanya vizuri? Kazi ya kocha huwa ni kuchangia mawazo tu kwa wachezaji wafanye hivi ama vile lakini kocha hamfundishi mtu kupiga chenga, kumiliki mpira na uwezo mwingine ndani ya uwanja bali huo ni uwezo wa MTU binafisi

Sasa kwa nini timu huhangaika kutafuta makocha tena kwa gharama kubwa?

Mimi ningezishauri timu za mpira zikitaka kufanya vizuri ziwe na uongozi imara wa timu tu, kisha kuwe na ukurasa wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa timu. Ukurasa huo utatoa fursa kwamashabiki na wadau wa timu kutoa maoni kwa wachezaji kabla na baada ya mechi na maoni hayo yatafanyiwa kazi na wachezaji pamoja na uongozi kwa matokeo chanya, na siyo kumpa mamlaka yote kufanya atakacho ambapo matokeo yake ni timu kufanya atakacho

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom