SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 1,213
- 1,918
Nimekuwa mtumiaji wa hii route ya KIGAMBONI mpaka KONGOWE kwa muda mrefu nikiwa na safari kati ya Kigamboni na Mkuranga. Kwa ujio wa safari za daladala kati ya KIGAMBONI na MWANDEGE nilipata ahueni ya nauli na muda..
Na hii route madereva na makonda wengi walikuwa wakiipigia kelele wakijifanya kuwa itakuwa na usaidizi kwa abiria na wao wakipata hela maana nauli mpaka MWANDEGE ni kubwa.. Lakini cha ajabu toka hii route imeanzishwa kumekuwa na usumbufu kwa abiria kwa ukatishwaji wa safari zinapofika KONGOWE,na hii inafanyika bila kujali muda. Yaani iwe asubuhi, mchana, jioni au usiku route zinakatwa. Ila ni mbaya zaidi zinapofika muda wa usiku.
Sehemu maarufu zinazotumiwa na daladala kujificha ni Barabara kwenda SERIKALI YA MTAA KONGOWE na barabara ya MTAA WA KICHANGANI..
Sasa kama hizi daladala hazitaki hii route kwanini waliziomba? Halafu uhuni mwingine ni kuchukua nauli ya kwenda MWANDEGE wakati wanaishia KONGOWE..
Na Traffic Police wa KONGOWE-MWISHO wanayaona haya madaladala yakikatisha safari na hawachukui hatua yoyote, Na SUMATRA nao wako kukimbizana na vibali vya bodaboda badala ya hawa wahuni.