Hivi trekta linalipa kwa kulima shamba lako au kukodisha?

Hivi trekta linalipa kwa kulima shamba lako au kukodisha?

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Wakuu kwema?

Mwaka huu baada ya kuuza mazao yangu natarajia kununua tracta kwa baje isiyo zidi Ml35

Kwa mwenye uzoefu tracta lina lipa zaidi kulima shamba lako binafsi au kukodishwa na kulima mashamba ya wengine?

Location yangu ni Singida Iramba ya Ndago

Nawasilisha

Cc okw BOBAN NSUNZU
 
Mimi nasubiria wadau watupe nondo; ila kunajamaangu anayotrecta huwa ananiambia nisinunue trecta nikitegemea kupata faida sana kwa kulimia mashamba ya watu(kukodishia) bali uwe na mashamba yako makubwa ndo utapata raha na faida ya kuwa na trecta
 
Lima ya kwako na ya wengine pia ukiweza simamia mwenyewe komaa mwenyewe linalipa. Kwa bei hio utapata used kwa kuagiza nje. Kwa mpya utapata HP 50.

Ukitaka mpya andaa 55 hadi 60 bila jembe unalipa 35 iliyobaki utalipa ndani ya mwaka mmoja au miwili. Trketa used nzuri ni ford, massey fiat.

Mpya utapata Massey, jondeer, new holland, deutz hizi ni mpya zero kilometa lakini ni manufactured India. Swaraj ni nzuri zinafanya Kazi nzuri Sana kibaigwa.

Nunua tretka kulingana na aina ya ardhi uliyopo na power HP kulingana na pesa haki na aina ya Kazi utakayo fanyia kama ni kulima mashamba yako tu na pesa haitoshi chukua HP 50. Kwa siku trekta inategemea na aina ya jembe, udongo, pia uendeshaji lakini si chini ya heka 20.

Kulima vizuri ni usiku au alfajiri hadi Saa tano asubui au kuanzia saa kumi jioni hadi Saa sita usiku mda wa wanga waachie mda wao hadi Saa kumi na moja wakimaliza Kazi zao endelea kulima.
 
Swaraj inapenda udongo mwepesi ila bei yake ni 35 million pamoja na jembe lake.. Kuna maeneo kama Kilindi-Tanga, Kibaigwa-dom, Kiteto-Manyara, baadhi ya maeneo ya Morogoro kwa Swaraj inafanya vizuri sana! Kwa huko uliko hapo ni valment, Massey, Ford, New Holland ila pia Kwa faida ya haraka tanguliza shamba lako hata hekari 400 hivi halafu piga vibarua vya kutosha.. faida itakuwa ya kutosha
 
Bro achana na mawazo ya trecta yanasumbua sana spea. Ninakushauri kama hiyo hela unayo basi nenda Dar au Mutukula tafuta fuso utanishukuru.
 
Bro achana na mawazo ya trecta yanasumbua sana spea.Ninakushauri kama hiyo hela unayo basi nenda dar au mutukula tafuta fuso utanishukuru
Trekta ni chombo kizuri sana kama wewe ni mkulima unaweza kulima mashamba Yako. Pia unawakodishia watu wengine. Ila nunua trekta mpya ndiyo utaona faida yake. Spea ziko nyingi tu, usiogope chapa kazi.
 
Swaraj inapenda udongo mwepesi ila bei yake ni 35 million pamoja na jembe lake.. Kuna maeneo kama Kilindi-Tanga, Kibaigwa-dom, Kiteto-Manyara, baadhi ya maeneo ya Morogoro kwa Swaraj inafanya vizuri sana! Kwa huko uliko hapo ni valment, Massey, Ford, New Holland ila pia Kwa faida ya haraka tanguliza shamba lako hata hekari 400 hivi halafu piga vibarua vya kutosha.. faida itakuwa ya kutosha
Sijaona Swaraj ya 35m sokoni..wewe uliona wapi
 
Ni sawa na kufungua kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti wakati hauna hata ekari moja ya alizeti

Swali, wakigoma kuleta alizeti yao wasikuletee ukamue, je utakamua nyuki waliogeuza mashine kuwa mzinga?
 
Okwi, Boban, Sunzu wee nunua trecta mbona Ndago watu now days wana kodi sana kwaajili ya kulima mashamba ya kule mbugani zinziligi,makunda na motomoto. Hata mashamba ya huku mtaani watu wana limia trecta siku hizi. Kuhusu ushauri wa trecta la kununua nunua kama lile la Generally Samweli Nkulu Massey Fugason [emoji16][emoji91]
 
Bei za Trekta ziko juu sana.
Bado utahitajika kununua majembe ya kulimia na ikiwezekana tela la kubebea zana za kazi nk.
Kwa wastani unatakiwa kuwa na mtaji wa m.100.
Halafu unaipeleka kijijini izalishe huku ghalama za uendeshaji zikizidi kuongezeka.
 
Okwi, Boban, Sunzu wee nunua trecta mbona Ndago watu now days wana kodi sana kwaajili ya kulima mashamba ya kule mbugani zinziligi,makunda na motomoto. Hata mashamba ya huku mtaani watu wana limia trecta siku hizi. Kuhusu ushauri wa trecta la kununua nunua kama lile la Generally Samweli Nkulu Massey Fugason [emoji16][emoji91]
Sasa mimi nalima ekari 100 za dengu Ndago na Mukulu, na wewe unayelima vibarua ekari 700 nani bingwa?! Weka hesabu zako vizuri mkuu Ismoo kisha uje tubishane hapa
 
Sasa mimi nalima ekari 100 za dengu Ndago na Mukulu, na wewe unayelima vibarua ekari 700 nani bingwa?! Weka hesabu zako vizuri mkuu Ismoo kisha uje tubishane hapa
Hakuna trekta ya kulima eka 700 vibarua kwa msimu mmoja,ukiwa na trekta ni heri uwe na shamba lako kabisa walau eka 200 au 300,utalima vibarua vichache kwa ajiri ya kupata hela ya kupalilia na kujazia mafuta kwa ajiri ya kulimia shamba lako.baada ya miaka mi5 itakuwa imenunua trekta nyingne.lkn trekta kupga vibarua tu inaweza chakaa na usijue hela imeenda wapi.
 
Kidogo umeongea.
Tatizo la kilimo ni hali ya hewa.
Unalima shamba kubwa mvua unakuwa kidogo, au maeneo mengine inanyesha kubwa sana na kuharibu mazao karibu yote.
Kilimo kina changamoto nyingi sana.
Pamoja na masoko.
 
Back
Top Bottom