Hivi tuko Mwaka gani?

Janjaweed upo sahihi, kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo tunavyozidi kurudi nyuma, tunapoteza mwelekeo as if ni meli ipo baharini haina rubani iliyopoteza dira inasombwa na upepo tu kadri mawimbi yanavyokuja kwa kasi.

Cha msigni sasa ni kuchukua hatua za haraka sana - ili tuendelee na safari yetu. kwa mfano ni kipi tulichokifanya cha kujivunia tangu wakoloni waondoke 1961? Mtu akisema "umoja wa kitaifa" upi? Uliogeuzwa kuwa mtaji wa wizi wa mali za umma harafu wengine wakae kimywa ili kulinda umoja na mshikamano huo eti.

Hatuwezi chochote why, tumelogwa na aliyetuloga kashakufa au? lazima tuanze revolution haraka sana - tunataka majibu yatokee October 2010.

Its our turn now that "We need a change that we can believe in" hayo uliyoandika nikisoma tena nahisi uchungu moyoni kwangu, this country bwana....mmmmhhh -watu wameifanya yao wenyewe...Come October we will see...
 

we taratibu aisee.. kuna usalama wa taifa humu😀
 
badala ye kwenda mbele tunarudi tuliko toka, muda si mreeefu tutawaita Waingereza kama sio Wajerumani tuwarudishie Nchi yao waiendeshe inaelekea walitukabidhi kwa makosa.
 
kwani Tangazania miaka uwa inaenda mbele au inarudi nyuma kama sio kubakia pale pale, wauleze wateja wa GTV na DECI washalipwa madai yao ndio utajua upo mwaka gani?
 
Kama unauliza majira, tupo mwaka 2010 ila kama nyakati ni wakati wa wapinzani kuvuna viti vingi vya ubunge na chama tawala(ccm) kupasuka kama kanu ya Kenya.
 
jamani hii ndiyo tanzania ya karne ya 21.Naomba muiangalie hii picha kwa makini sana than tuifanyie analysis na debate.
all the best.
 

Attachments

  • 01_10_fyz0h9[1].jpg
    890.7 KB · Views: 80
Kwa mbele kuna shangingi i guess Toyota Land Cruiser!Perhaps ni la mbunge au serikali.Thamani yake ,unaweza kununua cement na mabati kujenga shule hii.

We are like monkeys we dont care!
 
Taratibu jamani, vipaumbele ni vingi na wanakwenda taratibu, taking one at a time.

Wakati mwingine utegemeziw wetu nao umevuka mipaka. Kwa mfano kwenye hiyo shule - Uongozi wa kijiji umeshindwa kabisaaa kuitisha harambee na kuhamasisha wanakijiji kuvyafuta tofali na kuzichoma??

Kweli viongozi wetu ni 'reflection' ya sisi wenyewe. Kumbe mkuu wa kaya anapozunguka nje ya mipaka ya nchi yetu kutembeza bakuri la omba omba, anakuwa anawakilisha mindset yetu

Sio mpaka mkuu wa Mkoa afike hapo na viboko ndo viongozi husika wachukue hatua.

Kwa style hii, hatutafika popote na karne ya 25 itatukuta hapohapo
 

Wazazi wamechoka kutumikishwa...wao wao wajenge shule za msingi, wajenge sule za sekondary za Kata, wao wao wjenge zahanati, bado miundombinu ya maji...lazima wachimbe mifereji na mitaro ya kutandika bomba.

Serikali inafanya nn na fedha za wananchi? mm mlipa kodi, kodi yangu inafanya nn?

Wabunge wanapewa sijui mkopo au fedha za kununulia magari after every 5 yrs, regardless kama huyo mbunge amekuwa bungeni kwa 25 years = 5 periods. wanakamata pensions after 5 yrs na kurudi tena.

Wizara moja ina magari 30 HQ hapo bado mikoani, na yote sio less than 100M each.

Nachukia kusema hili, lakini kuna wakati tunakuwa kama manyani au mbuzi!!

aaaggrrrrrrrr
 
Siyo Tanzania tu...hata Nigeria, hata Central African Republic, hata Gambia, hata Zimbabwe na kwingineko kusini mwa Sahara kuna sehemu nyingi zilizo kama inavyoonekana kwenye hiyo picha
 


kumbuka wananchi hao watakuwa wakulima wa pamba au korosho au....serekali hiyo hiyo imeshindwa kuwatafutia soko la uhakika na kwa bei nzuri pesa watapata wapi hao wananchi??? lakujifunza hapa vipaumbele havimlengi mwananchi wa kawaida na mahitaji yake,magari ya kifahari kwanza au ni kujenga shule kwa ajili ya watoto wetu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…